The House of Favourite Newspapers

Burundi na DRC, Miongoni mwa nchi 12 za Afrika Zilizopewa Chanjo ya Malaria

0

Dozi milioni 18 za chanjo ya kwanza ya malaria, inayojulikana kama RTS,S, imesambazwa kwa nchi 12 za Afrika – ikiwa ni pamoja na Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – katika miaka miwili ijayo.

Takriban nchi 28 za Kiafrika zimesema zinataka chanjo hiyo ya malaria, lakini ni 14 pekee ndizo zimeliandikia shirika la kimataifa la kusambaza chanjo hiyo-Gavi, kuiomba.

Ghana, Malawi na Kenya zitakuwa za kwanza kupokea dozi hizi katika muda wa miezi mitatu ya mwisho ya mwaka huu.

Takriban kila dakika barani Afrika, mtoto wa chini ya umri wa miaka 5 hufa kutokana na malaria.

Wale wanaohitaji dozi milioni 18 za kwanza za chanjo ya RTS,S wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupokea chanjo hiyo.

Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO), Gavi na washirika wengine, walisema katika kutoa chanjo hiyo kwa kuzingatia nchi maskini zaidi, kunaweza kuleta mabadiliko makubwa na kwa wastani.

Nchi za Malawi, Ghana na Kenya, ambazo tayari zilikuwa zimetoa chanjo hiyo katika awamu ya majaribio kwa angalau watoto milioni 1.7, zilipokea dozi milioni 6.9 za chanjo hiyo.

Kwa mara ya kwanza, nchi nane – Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Benin, Uganda, Burkina Faso, Cameroon, Liberia na Sierra Leone – zitaanza kutoa chanjo ya malaria katika programu zao zilizopo.

Niger pia ni sehemu ya nchi zitakazopewa chanjo itakayotolewa.

Lakini Msumbiji na Sudan hazitapokea dozi zozote za chanjo hiyo, kutokana na kiwango kikubwa katika nchi hizo cha wale wanaokataa kutumia chanjo hiyo.

RTS,S ni chanjo ya kwanza kuidhinishwa kutumika dhidi ya malaria kwa watoto katika maeneo yenye maambukizi ya wastani hadi juu.

Leave A Reply