The House of Favourite Newspapers

Mgosi: Nyie chongeni tu, tunawafunga

0

Aplina Philipo,  Mbeya

NAHODHA wa Simba, Mussa  Hassan Mgosi, amesema kelele za mashabiki wa Mbeya City zimekuwa nyingi mitaani kila wanapopita, lakini ametamba kuwanyamazisha katika mchezo wao wa leo Jumamosi.

Mbeya City inaikaribisha Simba kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliojaa ushindani mkubwa kutokana na rekodi zao.

Simba haijawahi kuifunga Mbeya City kwenye uwanja huo tangu timu hiyo ilipopanda ligi kuu msimu wa 2013/14, kwani katika msimu huo zilitoka sare ya bao 1-1 na msimu uliopita wenyeji walishinda mabao 2-0.

Kikosi cha Simba kipo jijini Mbeya kwa wiki nzima sasa na kila wanapopita mitaani wamekuwa wakipokea ishara za kejeli ya kufungwa katika mchezo wa leo.

Mgosi aliliambia Championi Jumamosi: “Waache waongee wanavyotaka lakini wajue sisi tumetoka mbali kuja kushinda, hakuna shida, wao waongee, sisi tunawafunga kwa mara ya kwanza.”

“Najua wana wachezaji kama Boban (Haruna Moshi) na Kaseja (Juma), nawaheshimu sana kwani nimewahi kucheza nao lakini sasa kila mtu anaipigania timu yake.”

Leave A Reply