Bwalya Afungukia Ofa ya Waarabu

KIUNGO mshambuliaji wa Klabu ya Simba, Rally Bwalya amefunguka kuwa bado hajapewa taarifa yoyote ya kuhitajika na wababe wa soka la Morocco, Moulodia Oujda na anasubiri uongozi wa Simba juu ya dili hilo.

 

Vyanzo vya habari kutokea nchini Morocco vimeeleza kuwa klabu ya Moulidia imetuma ofa kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Simba, kwa ajili ya kuhitaji huduma ya kiungo huyo raia wa Zambia.

 

Bwalya aliyejiunga na Simba mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea, Power Dynamos ya Zambia amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja pekee.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Bwalya alisema: “Mpaka sasa binafsi sijawasiliana na klabu yoyote kuhusiana na ishu ya kuondoka Simba, lakini pia viongozi wangu hawajanipa taarifa ikiwa ikiwa kuna ofa yoyote kwa ajili yangu.

 

“Lakini masuala ya usajili ni maamuzi ya uongozi na kama kutakuwa na chochote kutoka huko Morocco au klabu nyingine basi wao wataweka wazi kila kitu.”

STORI: JOEL THOMAS NA CAREEN OSCAR


Toa comment