The House of Favourite Newspapers

Bwana Mdogo Vs Beer Tamu Mshindi Ni…

0

MAFAHARI wa muziki mjengoni YouTube hivi sasa ni Marioo ambaye anaongoza msafari wa wasanii wa Bongo na ngoma yake ya Beer Tamu.

Anayefuatia katika kushika usukani ni mkongwe wa Bongo Fleva , AliKiba ambaye anapewa kichwa na hit yake ya Bwana Mdogo.

Wasanii hawa wanakabana koo kileleni na Alikiba anaonekana amekubali kumpisha njia bwana mdogo wake Marioo aongoze kwa kuwa na watazamaji 1,420,875 ambao amewavuna tangu alipoachia wimbo wake Oktoba 29, 2021.

Alikiba anaonekana kumzidi watazamaji Marioo kwenye YoTube kwa kufikisha watu 1,869,673 tangu Oktoba 29, 2021 ngoma yake ya Bwana Mdogo ilipopeperuka hewani. Lakini ndiyo hivyo tena vigezo vya YouTube vimemfannya ashike nafasi ya pili.

Bila shaka nasi kama walaji wa burudani tutakuwa tumeona na kuzisikia ngoma hizi; mtazamo wetu ukoje kuhusu ngoma ya Bwana Mdogo na Beer Tamu ipi inatekenye moyo kwa sifa yoyote ile uwe mdundo, mpangilio au hata sauti na unenguaji?

Tupia maoni yako hapa!

@manyota_rich

Leave A Reply