The House of Favourite Newspapers

Bwanaharusi Afa Akienda Kufunga Ndoa!

0

afya (3) Maharusi siku ya send-off.

Stori: GABRIEL NG’OSHA, WIKIENDA

Mbeya: Inauma sana! Ma­jonzi yametawala mazishi ya bwana harusi, Gesson Ngassala aliye­fariki dunia kwa ajali akitokea Dar kwenda jijini Mbeya kwa ajili ya kufunga ndoa na mchumba’ke, Felister Ngowi anayedaiwa ni mjamzito.

afya (2)Kwa mujibu wa mmoja wa wana ndugu aliyezungumza na Wikienda, tukio hilo lilijiri Juni 21, mwaka huu baada ya Ngassala kumaliza send-off ya mchumba’ke huyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Kuala Lumpur uliopo Sinza-Kwaremy, Dar kisha kuamua kuelekea nyumbani kwao, Mbeya kwa ajili ya harusi ambayo ilikuwa ifanyike Juni, 23 mwaka huu.

Ilielezwa kuwa, akiwa njiani na zikiwa zimebaki saa kadhaa afunge ndoa ndipo akapata ajali eneo la Ilembula mkoani Iringa ambapo gari lake liliacha njia kisha kupinduka na yeye kufariki dunia.

afya (1)Bi harusi

BABA AZIMIA

Baada ya kutokea kwa tukio hilo, msamaria mwema alipiga simu kwa baba mzazi wa Ngassala na kumwambia kuwa mwanaye alikuwa amefariki dunia ambapo kutokana na taarifa hiyo, baba huyo alizimia kwa mshtuko.

MAMA ACHANGANYIKIWA

Habari zilieleza kuwa, mama mzazi wa marehemu naye aliposikia taarifa hizo mbaya za mwanaye alichanganyiwa asijue la kufanya.

RAFIKI YAO

Akizungumza kwa huzuni mmoja wa marafiki wa wachumba hao ambaye hakutaka jina kutajwa alisema: “Inauma sana. Mimi ni rafiki mkubwa wa Felister na nilimfahamu mchumba’ke tukiwa tunasoma Chuo cha Ualimu (TTC) Mpwapwa, Dodoma mwaka 2011 hadi 2013.

afya (4)Bwana Harusi

“Hata kwenye send-off yao iliyofanyika Sinza nilikuwepo.”

Wikienda lilimtafuta mmoja wa ndugu wa marehemu lakini simu yake iliita bila kupokelewa. Mwili wa marehemu Ngassala ulizikwa kwa simanzi kubwa kwani siku ya harusi ndiyo iligeuka ya mazishi, mwishoni mwa wiki iliyopita huko Kalobe-Iyunga, Mbeya.

Leave A Reply