The House of Favourite Newspapers

Breaking: Watoto 10 Wafariki Shule ya Byamungu Islamic Ikiteketea

0

BWENI la wavulana wa Shule ya Msingi Byamungu Islamic English Medium iliyopo Itera, Kyerwa, mkoani Kagera limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo, Septemba 14, 2020 na kusababisha vifo vya wanafunzi 10 na wengine sita wakijeruhiwa vibaya.

 

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Munaraka Muhammod, ambaye amewahi kufika katika eeo la tukio, amesema moto huo umeanza majira ya saa 9:20 usiku. Wanafunzi waliopoteza maisha ni kati ya umri wa miaka 6 hadi 12.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Rashid Mwaimu, amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo lakini mpaka sasa chanzo moto huo hakijafahamika.

 

Bweni hilo ni la watoto wadogo kati ya umri wa miaka 6 hadi 13, lilikuwa na wanafunzi 74,  ambapo watoto sita wamekimbizwa hospitalini ambapo watoto watatu hawajulikani walipo, wakihofiwa  huenda baado wamefunikwa katika kifusi cha bweni ambalo limeanguka.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, amewasili eneo la tukio, ambapo wakati akizungumza kwa njia ya simu amesema mbali na vifo hivyo pia kuna majeruhi saba, na kwamba ameunda tume itakayochunguza tukio hilo.

Leave A Reply