The House of Favourite Newspapers

Gwajima: Mimi si Kilaza, Sijaja Kuganga Njaa

0

Mgombea wa Ubunge Jimbo la Kawe, Dar es Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Askofu Josephat Gwajima amesema mwaka jana alitembelea nchi ya Marekani na watu wasifikiri kwamba yeye ni kilaza kwa sababu anaongea Kijapani, ameandika vitabau vitano vya Kijapani na vinauzwa kwenye mtandao maarufu duniani wa Amazon.

 

Gwajima amesema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni zake katika Jimbo la Kawe ambapo anakabiliana na upinzani mkali kutoka kwa aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo kwa miaka 10 kupitia Chadema, Halima James Mdee.

“Nikichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Kawe nitaweka Ambulance kwenye kila Kata, watu wangu watakimbizwa Hospitalini kwa haraka na jambo hili ni jepesi halihitaji Manispaa wala halihitaji Serikali.

 

“Nataka kufuta ile dhana ya kuwaza tunapata Askofu Mbunge, unapata chombo au mashine ya kusaga na kukoboa. Nawatumia salamu wanaomtukana Dkt. Magufuli.

 

“Sisi kwenye Ubunge hatukuja kuganga njaa, tumekuja kuwatumikia wananchi, tulishajaza makapu yetu tunataka tutoe kilichondani ya makapu pamoja na cha CCM tuwape Wananchi ili wawe na maisha mapya, tuone furaha tena Kawe,,” amesema Gwajima.

 

Aidha, Askofu Gwajima amesema akichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo ataweka Ambulance kwenye kila Kata, ili wananchi wake wapelekwe hospitali kwa haraka na kusisitiza jambo hili ni jepesi halihitaji Manispaa wala halihitaji Serikali.

 

Leave A Reply