The House of Favourite Newspapers

CAG: EWURA Imepoteza Lita Bil 1.4 za Petroli

0


MAMLAKA ya Usimamizi wa Nishati na Maji (EWURA) imeshindwa kuthibitisha matumizi ya lita bilioni 1.4 zilizoingia nchini kwa miaka mitatu na kusababisha Mamlaka ya Mapato (TRA) kukosa kodi na tozo ya nishati hiyo.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, amesema EWURA haikuzitumia ipasavyo kanuni zake za udhibiti hivyo kushindwa kung’amua matumizi ya lita hizo za petroli.

Utaratibu wa udhibiti unataka bidhaa zote za petroli zilizoingizwa nchini kwa matumizi ya ndani kuthibitishwa na kuwekwa alama isipokuwa zilizosamehewa kodi.

Pia, amesema amebaini mamlaka hiyo haina utaratibu unaoiwezesha kugundua chanzo cha tofauti iliyoonekana na hii inaashiria udhaifu katika ufuatiliaji wa bidhaa zinazoingia nchini kwa matumizi ya ndani, jambo linaloweza kusababisha upotevu wa mapato.

Leave A Reply