The House of Favourite Newspapers

Uwanja wa Azam Wateketeza Bilioni Tano

0

BAADA ya timu ya Azam FC kukamilisha ujenzi wa uwanja wao eneo la kuchezea, uongozi wa timu hiyo umesema kuwa umetumia shilingi bilioni tano kukamilisha ujenzi huo kwa kipindi cha miezi miwili.

Uwanja huo ambao ulianza kufanyiwa marekebisho mwishoni mwa mwaka jana kwa kubadilisha kapeti sehemu ya kuchezea ambalo limeisha muda wake kufuatia kuwekwa mwaka 2009.

 

Kwa sasa unaonekana kuwa wa kisasa zaidi.Akizungumza na Championi Jumatano, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’, alisema kuwa marekebisho hayo yaliyofanyika kwa kipindi cha miezi miwili yamegharimu shilingi bilioni tano ikiwa ni katika eneo la kuchezea peke yake.

 

“Mkakati wetu ulikuwa kurekebisha katika eneo la kuchezea yaani kuondoa ile kapeti ya zamani ambayo ilikuwa imeshapita muda wake kwa sababu ilitakiwa kutumika katika kipindi cha miaka kumi ambacho kimeshafi kia na ndiyo maana marekebisho yote yamehusu eneo la kuchezea.

 

“Sasa ukiangalia eneo la kuchezea tumeshamaliza matengenezo yake ikiwa na tofauti ya teknolojia kubwa ambayo imetumika kwa lengo la kufanya uwanja kuwa bora na wa kisasa, lakini kwa upande wa gharama za matengenezo yote zinafi ka bilioni tano kuanzia nyasi na vifaa vyote ambavyo vimetumika maana kama nyasi kodi yake ni kubwa mno,” alisema Zaka Zakazi.

Stori na Ibrahim Mussa na Abdulghafal Ally, Dar

MSHINDI BSS HAJALIPWA PESA ZAKE, WAZIRI SHONZA AMLIPUA MADAM RITHA

Leave A Reply