The House of Favourite Newspapers

Cameroon Ndiyo Mabingwa wa AFCON 2017

GABON: Usiku wa kuamkia leo, Timu ya Taifa ya Cameroon wamefanikiwa kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2017‘ baada ya kuisambaratisha Misri kwa bao 2-1 nchini Gabon. Cameroon wameweka rekodi ya kuchukua kombe hilo mara 5 sasa huku wakifuta uteja kwa kufungwa fainali mbili na Misri.

Waliokuwa wa kwanza kufunga ni Misri kunako dakika ya 22 kupitia kwa Mohamed Elneny. Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Misri 1-0 Cameroon.

Kunako kipindi cha pili Cameroon waliingia na moto mkali na kufanikiwa kupata bao la kusawadhisha kupitia kwa Nicolas N’koulou kunako dakika ya dakika ya 58 huku Vincent Aboubakar akiihakikishia ushindi Cameroon kwa kupachika bao la ushiondi dakika ya 88.

Ushindi huo unakuja baada ya Cameroon kufumgwa fainali mbili za AFCON na Misri, alifungwa fainali ya AFCON 2008 goli 1-0 Mohamed Aboutrika akifunga goli hilo, lakini walipoteza fainali ya AFCON 1986, Cameroon wanakuwa wamechukua taji lao la tano la AFCON wakati Misri wanabakia na rekodi yao ya kuchukua mataji nane ya AFCON.

Rekodi nyingine zilizowekwa katika AFCON na Cameroon ni kuwa inakuwa timu ya kwanza kuwahi kuifunga Misri goli katika fainali za AFCON baada ya Ethiopia, huku kocha wa Misri Hector Raul  Cuper akiendeleza rekodi yake mbovu kwa kupoteza fainali yake ya sita katika soka akiwa kama kocha wa timu tofauti.

Kwa stori zote kali, Tu-follow

Facebook @Globalpublishers

Twitter @GlobalHabari

Instagram @GlobalPublishers

YouTube @GlobalTVTZ

 

EPL: Chelsea 2-0 Arsenal

Comments are closed.