The House of Favourite Newspapers

Khadija Kopa: Nina Zawadi ya Kuwapa Wapendanao, Dar Live

IJUMAA WIKIENDA | Over Ze Weekend

ZIKIWA zimesalia siku kadhaa kufikia Februari 14, am­bayo ni Sikukuu ya Wapendan­ao ‘Valentine’s Day’ Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa amewaambia mashabiki watakaojitokeza ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar kuwa, siku hiyo atakuwa na zawadi maalum kwao.

Akizungumza na Over Ze Weekend, Khadija Kopa ambaye pia ni kiongozi wa Bendi ya TOT Taarab alisema kuwa, mbali na kutoa zawadi nyingi ambazo ni sapraizi kwa mashabiki, usiku huo pia mashabiki watarajie kusikia nyimbo zake zote kali.

Khadija Kopa akitumbuiza

“Kwanza nina zawadi kubwa ya kuwapa wapendanao wote wataka­ofika Dar Live ambayo kwa sasa ni siri yangu. Pia nitaporomosha vibao vyote kuanzia Mjini Chuo Kikuu, Fahari ya Mwanamke na nyingine nyingi,” alisema Kopa.

Naye Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema mbali na uwepo wa Kopa, mashabiki watamshuhudia mkongwe wa Taarab kutoka East Africa Modern, Bi Mwanahawa Ally anayetamba na vibao vingi Wakerekwao, Wema na Roho Mbaya Haijengi.

“Wote tunamjua Bi Mwana­hawa stejini yupoje. Niwaombe mje kwa wingi kushuhudia mtifuano wa aina yake mbele ya wapendanao,” alisema Mbizo na kumalizia kuwa, usiku huo wapendano 100 wa kwanza wa­takaopendeza watapata zawadi spesho.

Kwa stori zote kali, Tu-follow

Facebook @Globalpublishers

Twitter @GlobalHabari

Instagram @GlobalPublishers

YouTube @GlobalTVTZ

Save

Comments are closed.