The House of Favourite Newspapers

Cameroon Yaigonga Ghana na Kuifuata Misri Fainali ya Afcon

TIMU ya Taifa ya Cameroon imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Mataifa Afrika maarufu kama Afcon baada ya kuinyuka Ghana kwa mabao 2-0 katika mechi ya pili ya nusu fainali.

Ilikuwa mechi ngumu tokea mwanzo na mapumziko ilikuwa ni sare ya bila kufungana. Ngadeu Ngadjui aliiifungia Ghana bao katika dakika ya 72 baada ya uzembe wa mabeki wa Ghana lakini wakati inaonekana kama Ghana watasawazisha, Cameroon wakamaliza kazi kupitia kwa Christian Bassogog.
Cameroon sasa watamenyana Misri kwenye mechi ya fainali hizo itakayofanyika Jumapili, Februari 5, 2017 saa 4:00 usiku.

 

Kwa stori zote kali, Tu-follow

Facebook @Globalpublishers

Twitter @GlobalHabari

Instagram @GlobalPublishers

YouTube @GlobalTVTZ

 

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Save

Save

Comments are closed.