The House of Favourite Newspapers

Wee Sanch, Ndo’ Tuseme Biashara Matangazo?

@Sanchworld
 Janeikunda Evarist Rimoy, a.k.a Sanchoka au Sanchi – @sanchiworld

 Stori: Na OJUKU ABRAHAM | IJUMAA | ZA CHEMBE LAZIMA UKAE

Ni binti mmoja mrefu, mwenye mwili wa kisichana hasa na anastahili kuitwa mrembo. Ameamua kuchafua fani ya uanamitindo, moja ya sanaa zinazolipa zaidi katika ulimwengu wa wanawake.

Jane Rimoy ‘Sanch’

Sanchoka ‘Sanch’, ndilo jina lake maarufu zaidi hapa Bongo licha ya jina lake halisi kuwa ni Janeikunda Rimoy. Kwa jinsi umbo lake lilivyo, hasa kuanzia kiunoni kwenda chini, baadhi walimhusisha na ile tabia ya mabinti wengi wa Kibongo kutumia dawa za Kichina zenye kuongeza ukubwa wa makalio, matiti na hips.

Kabla sijaonana naye uso kwa uso, niliamini hivyo maana kuna wasichana wengi ninaowafahamu wamejitunisha na madawa hayo ya kuongeza maumbile yao kiasi hivi sasa wanajuta. Yes, alikuja ofisini kwetu na nikawa miongoni mwa walioomba kujua ukweli kuhusu umbo lake.

Ni orijino, yaani hadi siku ile wiki chache zilizopita, alikuwa na umbo lake la asili kabisa. Na kwa wanaopenda asili, ama kwa hakika ni lazima wavutike mbele ya huyu dada. Na cha kufurahisha, nilimuuliza kama huwa anapata kero kwa kiasi gani kutoka kwa wanaume wakware, akaniambia kwa wastani, anapokea kati ya simu 25 hadi 30 kwa siku, zote hizo akitongozwa!

Swali langu lilitokana na uvumi kuwa mwanamitindo huyu chipukizi ni miongoni mwa akina dada wanaojirahisi kwa mapedeshee wa mjini. Alikataa katakata, kwamba hajawahi na hawezi poteza thamani ya utu wake kwa sababu ya pesa.

Nilimuamini kwa sababu kujirahisi ni tabia ya mtu, haitokani na umbo wala sehemu ulipo. Lakini kwa namna ya kushangaza sana, wiki chache zilizopita, katika mitandao ya kijamii, nilikutana na picha yake ya video, akionyesha makalio yake kwa namna ya kuwaonyesha watu wamuone jinsi ‘alivyojaaliwa’.

Nikafahamu huenda ni utoto tu unamsumbua, kwamba akikua ataacha, maana kwa mujibu wake, umri wake upo chini ya miaka 25. Ghafla, juzikati, nakutana na clip nyingine ya video, safari hii, akipekecha matiti yake kwa namna ya kuwaonyesha watu, jinsi gani yalivyo na mvuto!

Sanch, siku zote ni mtu wa kula bata viwanjani

Huu siyo utoto, huu ni mkakati wenye malengo maalum. Mtoto wa kike mwenye kujiheshimu unawezaje kupiga picha za kijinga kama hizi na kuzitupia kwenye mitandao ya kijamii? Watoto wa mjini wanasema biashara matangazo. Ni vigumu kuukataa msemo huu unapomuangalia mtu kama Sanch na namna video zake hizo zilivyopigwa.

Kwa binti kama yeye, hivi sasa angekuwa na mchumba wake wa maana anasubiri siku wayamalize, iwe kwa sheikh, padre au mchungaji, lakini anapokuwa amekosa mtu wa namna hiyo, ni dhahiri kuwa kuna mambo hayaendi sawa sehemu fulani katika maisha yake.

Na huenda, yanachangiwa kwa kiwango kikubwa na tabia yake hii ambayo sasa ameamua kuionyesha kwa watu wasio karibu naye. Kwa sababu haiwezekani, mtu aliye mchumba wa mtu, akapiga video kama ile na kuitupia mitandaoni. Na hata kama hajachumbiwa, bado binti mwenye maadili mema, tena mwenye shepu kama Sanch, hawezi kufanya vile, kwani tafsiri ya haraka ya watu ni kuwa anajiuza!

Sanchi katika pozi la kula upepo mwanana

Ni vigumu kujua kwa nini amekuwa namna hiyo, maana wengine wanadhani maisha magumu, labda ana tamaa ya vitu vizuri vinavyohitaji fedha na kadhalika. Vyovyote itakavyokuwa, ni fedheha kwake na familia yake kwa kile kilichotokea mitandaoni.

Sanch, katika moja ya mapozi yake matata

Msichana anayejinadi mitandaoni ana nafasi kubwa zaidi ya kupoteza mwelekeo wa maisha yake kuliko kufanikiwa. Chunga nyendo zako Sanch!

 

Kwa stori zote kali, Tu-follow

Facebook @Globalpublishers

Twitter @GlobalHabari

Instagram @GlobalPublishers

YouTube @GlobalTVTZ

 

Sanchi; Staa Mwenye Figa Bomba Kuliko Wote Bongo, Aeleza Sifa za Mwanaume Anaemtaka

 

Save

Comments are closed.