The House of Favourite Newspapers

Canada Yazindua mpango wa uhamiaji kuvutia Wataalamu Wenye Ujuzi

0
Visa application form, passport and flag of Canada

H-1B visa ni kwa ajili ya wafanyakazi wa kigeni wasio wahamiaji na wenye ujuzi maalum. Kuanzia Julai 16 watu hadi 10,000 wenye visa za aina hii wanaweza kuomba kufanya kazi nchini Canada. Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati mpya nchini humo wa Tech Talent Strategy.

Canada imezindua mpango wa uhamiaji ili kuvutia wataalamu wenye ujuzi wa teknolojia kutoka Marekani na wenye visa za kazi za H-1B.

H-1B visa ni kwa ajili ya wafanyakazi wa kigeni wasio wahamiaji na wenye ujuzi maalum. Kuanzia Julai 16 watu hadi 10,000 wenye visa za aina hiyo wanaweza kuomba kufanya kazi nchini Canada. Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati mpya nchini humo wa Tech Talent Strategy.

“Serikali ya Canada inakubali jukumu linalojitokeza la Canada kama kiongozi katika kuajiri vipaji vya teknolojia ya kimataifa na kuwa kivutio ili kuhakikisha Canada sio tu inajaza kazi zinazohitajika leo, lakini pia kuvutia ujuzi na vipaji vya biashara ili kubuni ajira za kesho,” taarifa iliyotolewa na kitengo cha Uhamiaji, Wakimbizi na Uraia Canada ilisema.

Hii inafuatia tangazo la Novemba ambapo serikali iliweka lengo la kukabiliana na uhaba wa ajira unaokaribia. Ifikapo mwaka 2025, nchi inataka kuwakaribisha wahamiaji milioni 1.45 ikiwalenga watu wanaotoa mafunzo katika huduma za afya na ujuzi mwingine wa ajira unaohitajika, na kupata wafanyakazi wenye ujuzi kwenye sekta muhimu za uchumi wake.

Leave A Reply