The House of Favourite Newspapers

Cannavaro ashusha presha Yanga, aitaka Simba SC

0

cannavaro-FILEminimizer.jpg

Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

Wilbert Molandi, Dar es Salaam

HABARI njema kwa mashabiki wa Yanga ni kuwa nahodha, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema mashabiki wa timu hiyo wasiwe na hofu kuwa atakuwa fiti kwenye mchezo dhidi ya Simba.

Taarifa hizo, huenda zikamshtua kocha msaidizi wa Simba Mganda, Jackson Mayanja na mashabiki wa timu hiyo wakati Kelvin Yondani akiitumikia adhabu ya kadi aliyopewa kwenye mechi dhidi ya Coastal Union, Cannavaro anarejea uwanjani.

Cannavaro ambaye alisema ana asilimia 80 ya kucheza mechi ya Simba kutokana na na maendeleo yake tayari ameshaanza mazoezi mepesi jijini Dar wakati wenzake wakiwa mkoani Mbeya.

“Ninajua mashabiki wa Yanga hivi sasa watakuwa kwenye hofu kubwa kutokuwepo kwa Yondani kwenye mechi na Simba baada ya kupewa kadi nyekundu.

“Naomba niwatoe hofu katika hilo, kikubwa ninashukuru hivi sasa ninaendelea vizuri, kama mazoezi mepesi tayari nimeanza na nitaungana na wenzangu wakirejea kutoka Mbeya.

“Wiki moja inanitosha kabisa kujiweka fiti na naamini kuwa naweza kuwazuia Simba wasilete madhara langoni kwetu,” alisema Cannavaro.

Leave A Reply