Carlinhos Arejeshwa Yanga, Kuanza Mazoezi

KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze, amesema kuwa kiungo wa timu hiyo, Carlos Sténio Carlinhos anatarajia kurejea kikosini kuungana na wenzake baada ya majeraha yake kuendelea vizuri.

 

Kaze alisema baada ya kiungo huyo kukaa nje kwa wiki kadhaa sasa yupo tayari kuanza mazoezi mepesi, ikiwemo kwenda Gym na kufuata programu ya madaktari kisha baada ya hapo ataanza programu nyingine kwa ajili ya maandalizi ligi kuu.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Kaze alisema majeraha ya Carlinhos yalikuwa yanakwenda sawa na ndiyo maana aliamua kumuondoa kwenye kikosi kilichoshiriki mashindano ya Kombe la Mapinduzi ili apate muda wa kuwa fiti zaidi, jambo ambalo limesaidia na sasa yupo tayari kuipigania timu kwenye raundi hii ya pili.

 

“Tunategemea kuwa Carlinhos ataanza mazoezi wiki hii kwani ripoti ya madaktari ilionyesha kuwa anaweza kuanzia Gym.

Kisha baada ya muda ataungana na wenzake kwenye mazoezi ya pamoja kujiandaa na michezo ya ligi kuu,” alisema Kaze.Nyota huyo raia wa Angola aliumia kwa mara ya Oktoba 19, kwenye mazoezi ya timu yaliyofanyika Kigamboni jambo lililopelekea akose michezo kadhaa.

Stori: Issa Liponda, Dar es SalaamTecno


Toa comment