The House of Favourite Newspapers

CCM Yaipongeza ACT Wazalendo – Video

0

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimekipongeza Chama cha ACT Wazalendo kwa kuibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha Ubunge katika Jimbo la Konde Visiwani Pemba na kukibwaga CCM.

 

Hayo9 yamesemwa leo Jumanne, Oktoba 12, 2021 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka, wakati akizungumza na wanahabari jijini Dodoma.

 

“Chama cha Mapinduzi kinakipongeza ACT Wazalendo kwa kushinda katika jimbo la Konde, Wilaya ya Micheweni mkoani Kaskazini Pemba na hiyo ndio siasa safi. Kumalizika kwa chaguzi hizi ndogo za udiwani na ubunge majimbo ya Konde na Ushetu kwetu kumetupa funzo kwa wenzetu katika uso wa demokrasia.

 

“Rais Samia Suluhu ameendelea kusimamia na kiuimarisha haki za binadamu, usawa, demokrasia, kupinga aina zote za ubaguzi pamoja na kupiga vita ubadhirifu. Katika kujenga na kukuza uchumi serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Samia imeendelea kuweka mazingira wezeshi ya kuvutia uwekezaji.

 

“Chama cha Mapinduzi kinaendelea kuwaomba na kuwahamasisha wananchi wote kuendelea kumuunga mkono Rais Samia, Rais ambaye ana dhamira njema ya kutaka kutufikisha kule tunakotaka na kudumisha huduma za msingi za jamii ikiwemo afya, maji, elimu.

 

“Chama Cha Mapinduzi kinatoa wito kwa wanachama na kamati za siasa za ngazi zote kuhakikisha kwamba wanafuatilia kwa karibu sana utekelezaji wa mradi wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uviko-19 kuhakikisha hakuna fedha zinaliwa.

 

“Fedha za mradi wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uviko-19 si sadaka bali zimekuja kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania. Fedha zimekuja kwa ajili ya kuwaletea maendeleo ya Watanzania na kuhakikisha uchumi wa mtu mmoja mmoja unainuka.

 

“Nichukue Fursa hii kuipongeza sana wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kupitia kwa waziri Ummy Mwalimu kwa kazi nzuri ya kusimamia maelekezo ya Mhe Rais Samia na sisi Chama tunaendelea kusisitiza fedha hizi sio sadaka zimekuja kwa ajili ya Maendeleo ya Watanzania.

 

“CCM ni chama kikubwa katika mambo ambayo CCM iko nayo makini ni mambo ambayo yanayobeba maslahi mapana ya CCM na ndio sababu inaendelea kusalia madarakani. Kwa yeyote ambaye aliyekwenda kinyume na taratibu, taratibu zake zipo na zitafuatwa.

 

“CCM ndio inaunda dola na kupewa dhamana ya uongozi, tumekuwa tukipita na kuangalia miradi na kusema hapa tumeridhika na hapa hatujaridhika na kutaka hatua zichukuliwe, tunafanya hivyo kwa kuwa sisi ndio tumebeba dhamana na maslahi ya serikali,” amesema Shaka Hamdu Shaka.

Leave A Reply