The House of Favourite Newspapers

CCM yashinda majimbo 159, Chadema majimbo 35

0

bungeniCHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeongoza kwa kunyakua majimbo ya uchaguzi 159, ambayo hadi jana yamethibitishwa na wasimamizi waliopewa mamlaka ya kutangaza matokeo hayo na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikifuatia kwa kupata majimbo 35.

Aidha, wanawake wengi wameonekana kufanya vizuri katika uchaguzi wa ubunge na hadi sasa waliotajwa na kuthibitishwa kushinda katika majimbo waliyogombea wamefikia wanawake 19 na idadi hiyo inaweza kuongezeka.

Hata hivyo, hayo si majimbo yote ambayo vyama hivyo vimefanikiwa kushinda, kutokana na baadhi ya majimbo bado matokeo yaliyoonesha utata, yanaendelea kuhesabiwa na kutangazwa pale inapoonekana inafaa.

Aidha, katika uchaguzi huo, Chama cha Wananchi (CUF) nacho kimefanikiwa kupata majimbo 17 huku Chama cha NCCR-Mageuzi na ACT-Maendeleo vyote vikipata jimbo moja moja. Jumla ya majimbo yote ya uchaguzi ni 264 na yaliyokwishatangazwa hadi sasa ni majimbo 207.

Katika upembuzi wa majimbo hayo uliofanywa na gazeti hili, baada ya kuthibitishwa, CCM imepata majimbo ya Busega (Raphael Chegeni), Nyamagana (Stanslaus Mabula), Msalala (Ezekiel Maige), Ngara (Alex Gashaza), Kigamboni (Faustine Ndugulile), Kishapu (Suleiman Nchambi) na Kisarawe (Suleiman Jaffo).

Majimbo mengine ni Bagamoyo (Dk Shukuru Kawamba), Ilemela (Angelina Mabula), Ilala (Mussa Azzan ‘Zungu’), Singida Mjini (Mussa Sima), Same Magharibi (Dk Mathayo David Mathayo), Rungwe (Saul Amon), Mbogwe (Augustino Masele), Chalinze (Ridhiwani Kikwete), Iramba Magharibi (Mwigulu Nchemba) na Hanang (Dk Mary Nagu).

Aidha, majimbo mengine ni Njombe Kaskazini (Joram Hongoli), Dodoma Mjini (Antony Mavunde), Mtama (Nape Nnauye), Babati Vijijini (Jitu Soni), Kahama Mjini (Jumanne Kishimba), Sikonge (George Kakunda), Nzega Mjini (Hussein Bashe), Urambo (Margaret Sitta), Mpanda Vijijini (Moshi Kakoso) na Geita Mjini (Constantine Kanyasu).

Chama hicho pia kilijipatia ushindi katika majimbo ya Mbeya Vijijini (Oran Njeza), Mafinga Mjini (Cosato Chumi), Kalenga (Godfrey Mgimwa), Isimani (William Lukuvi), Songea Mjini (Leonidas Gama), Mkalama (Allan Kiula), Newala (George Mkuchika), Kavuu (Dk Prudenciana Kikwembe) na Kwimba (Mansoor Shanif).

Mengine ni Bukoba Vijijini (Jason Rweikiza), Nyasa (Stella Manyanya), Kondoa Mjini (Edwin Sanda), Kondoa Vijijini (Dk Kashatu Kijaji), Chemba (Juma Nkamia), Chamwino (Joel Mwaka), Mtera (Livingstone Lusinde), Bahi (Omar Baduel), Mpwapwa (George Lubeleje), Kibakwe (George Simbachawene) na Kongwa (Job Ndugai).

CCM pia imepata Sengerema (William Ngeleja), Maswa Mashariki (Stanslaus Nyongo), Maswa Magharibi (Mshimba Ndaki), Itilima (Njalu Silanga), Bariadi (Andrew Chenge), Meatu (Salum Hamis), Muheza (Balozi Adadi Rajabu), Kasulu Mjini (Daniel Nsanzugwanko), Buhigwe (Albert Ntabaliba), Handeni Vijijini (Mboni Mhita) na Morogoro Mjini (Abdulaziz Abood).

Gairo (Ahmed Shabiby), Rorya (Lameck Airo), Ngorongoro (William Ole Nasha), Mvomero (Suleiman Murad), Morogoro Kusini Mashariki (Mgumba Omary), Morogoro Kusini (Prosper Mbena), Nkasi Kusini (Deuderius Mipata), Nkasi Kaskazini (Ally Keissy), Singida Kaskazini (Lazaro Nyalandu), Singida Magharibi (Elibariki Kingu) na Igunga (Dk Dalaly Kafumu).

Mengine yaliyoenda CCM ni Solwa (Ahmed Salum), Katavi (Issac Kamwele), Mpanda Mjini (Sebastian Kapufi), Mpanda Vijijini (Moshi Kakoso), Nsimbo (Richard Mbogo), Ruangwa (Kassim Majaliwa), Sumbawanga Mjini (Aeshi Hilaly), Kyela (Dk Harrison Mwakyembe), Ileje (Janeth Mbene) na Mbarali (Pirmohamed Mulla).

Majimbo mengine yaliyochukuliwa na chama hicho ni Busokelo (Atupele Mwakibete), Vwawa (Japhet Hasunga), Lupa (Victor Mwambalaswa), Songwe (Philipo Mulugo), Madaba (Joseph Mhagama), Peramiho (Jenista Mhagama), Kilosa Kati (Mohamed Bawazir), Kiteto (Emanuel Papian), Mbulu (Paul Isaay) na Karagwe (Innocent Bashungwa).

Kyerwa (Innocent Bilakwate), Nkenge (Dk Diodorus Kamala), Muleba Kusini (Profesa Anna Tibaijuka), Muleba Kaskazini (Charles Mwijage), Biharamulo Magharibi (Mukasa Oscar), Mwibara (Kangi Lugola), Bunda Vijijini (Boniphace Getere), Makete (Dk Norman Sigala), Kibaha Vijijini (Hamoud Jumaa) na Sumve (Richard Ndassa).

Magu (Kiswaga Destery), Chato (Dk Merdad Kalemani), Nzega Vijijini (Dk Khamis Kigwangallah), Njombe Mjini (Edward Mwalongo), Mwanga (Profesa Jumanne Maghembe), Nyangh’wale (Hussein Kassu), Newala Vijijini (Rashid Akbal), Butiama (Nimrod Mkono), Korogwe Vijijini (Stephen Ngonyani) na Korogwe Mjini (Mary Chatanda).

Misungwi (Charles Kitwanga), Busanda (Lolensia Bukwimba), Manonga (Seif Gulamali), Tabora Mjini (Emmanuel Mwakasaka), Mlalo (Rashid Shangazi), Kisesa (Luhaga Mpina), Lindi Mjini (Selemani Kaunje), Mkinga (Dustan Kitandula), Mbinga Mjini (Sixtus Mapunda), Mbinga Vijijini (Martin Msuha) na Musoma Mjini (Vedastus Mathayo).

Mengine ni Geita Vijijini (Joseph Kasheku), Kibaha Mjini (Silvestry Koka), Bukombe (Dotto Biteko), Shinyanga Mjini (Steven Masele), Msalala (Ezekiel Maige), Pangani (Jumaa Aweso), Mufindi Kaskazini (Mahamoud Mgimwa), Mufindi Kusini (Mendrad Kigola), Kilolo (Venance Mwamoto) na Maswa Mashariki (Stanslaus Nyongo).

Maswa Magharibi (Mashimba Ndaki), Chilonwa (Joel Mwaka), Mtwara Vijijini (Hawa Ghasia), Nanyamba (Abdallah Chikota), Tunduru Kusini (Daimu Mpakate), Tunduru Kaskazini (Ramo Makani), Bunda Vijijini (Boniface Mgetere), Mkuranga (Abdallah Ulega) na Mbulu Vijijini (Gregory Massay) nayo yameenda CCM.

Mengine ni Mbulu Mjini (Zacharia Paul), Kilindi (Kigua Mohamed), Namtumbo (Edwin Ngonyani), Ushetu (Elias Kuandikwa), Bumbuli (January Makamba), Segerea (Bonnah Kaluwa), Kalambo (Josephat Kandege), Wanging’ombe (Gerson Lwenge), Kigoma Kaskazini (Peter Serukamba), Muhambwe (Justus Nditiye), Kasulu Vijijini (Agustie Vuma) na Kilolo (Venance Mwamoto).

Kwa upande wa Chadema, hadi sasa kimejinyakulia majimbo 35 ambayo ni Kibamba (John Mnyika), Mikumi (Joseph Haule), Bukoba Mjini (Wilfred Lwakatare), Same Mashariki (Nagenjwa Kayoboka), Rombo (Joseph Selasini), Bunda Mjini (Ester Bulaya), Hai (Freeman Mbowe) na Mbeya Mjini (Joseph Mbilinyi).

Majimbo mengine ni Kawe (Halima James Mdee), Longido (Onesmo Nangole), Ukonga (Waitara Mwita), Mlimba (Suzan Kiwanga), Singida Mashariki (Tundu Lissu), Ubungo (Said Kubenea), Mbozi (Paschal Haonga), Tunduma (Frank Mwakajoka), Momba (David Silinde), Kilombero (Peter Lijualikali) na Karatu (Willy Qambalo).

Aidha, chama hicho kilishinda katika majimbo ya Simanjiro (James ole Millya), Arumeru Magharibi (Gipson ole Meseyeki), Tarime Mjini (Ester Matiko), Siha (Godwin Mollel), Buyungu (Kasuku Bilago), Monduli (Julius Kalanga), Arumeru Mashariki (Joshua Nassari), Serengeti (Marwa Ryoba) na Babati Mjini (Pauline Gekul).

Mengine ni Moshi Mjini (Jaffar Michael), Tarime Vijijini (John Heche), Iringa Mjini (Peter Msigwa), Ndanda (Cecil Mwambe) na Moshi Vijijini (Anthony Komu). CUF yenyewe hadi sasa kina majimbo 17 ambayo ni Temeke (Abdallah Mtolea), Mchinga (Hamidu Bobali), Kilwa Kusini (Said Bungala), Kaliua (Magdalena Sakaya), Tandahimba (Ahmad Katani), Mtwara Mjini (Maftaha Nachuma), Kinondoni (Maulid Mtulia), Kilwa Kaskazini (Vedasto Ngombale) na Tanga Mjini (Musa Mbaruk).

Majimbo mengine ni Wawi, Chakechake, Ole, Ziwani, Kojani, Gando, Wete na Mgogono. Wanawake waliong’ara hadi sasa majimboni ni Kaliua (Magdalena Sakaya), Babati Mjini (Pauline Gekul), Hanang (Mary Nagu), Urambo (Margaret Sitta), Kavuu (Dk Prudenciana Kikwembe), Nyasa (Stella Manyanya), Handeni Vijijini (Mboni Mhita), Ileje (Janeth Mbene), Peramiho (Jenista Mhagama) na Muleba Kusini (Profesa Anna Tibaijuka).

Wengine ni Busanda (Lolensia Bukwimba), Mtwara Vijijini (Hawa Ghasia), Segerea (Bonnah Kaluwa), Same Mashariki (Nagenjwa Kayoboka), Bunda Mjini (Ester Bulaya), Kawe (Halima James Mdee), Mlimba (Suzan Kiwanga), Tarime Mjini (Ester Matiko) na Kaliua (Magdalena Sakaya).

Leave A Reply