The House of Favourite Newspapers

Hawa Ndo Mapacha Warembo Zaidi Duniani

 

WATOTO mapacha wenye umri wa miaka nane, Leah Rose na  Ava Marie,  wametajwa kuwa ndiyo mapacha na mamodo wenye mvuto mzuri zaidi na wenye mashabiki wengi zaidi duniani ambapo akaunti yao ya Instagram ikiwa inatambulika (tiki ya bluu).

 

Mapacha hao walizaliwa Julai 7 mwaka 2010 huko Carlifonia, Marekani,  na wazazi wao ambao ni  Jaqi na Kevin Clements.

 

 

Jaqi aliwapeleka mapacha hao kuwaandikisha kwenye umodo walipofikisha muda wa miezi sita lakini, hata hivyo, akaona huo haukuwa muda maalumu.

 

 

Ilipofika Julai mwaka 2017 ndipo alipotambua  kwamba wanawe walikuwa na utashi upi, hii ni baada ya kupost picha katika akaunti yao ya Instagram aliyowafungulia ambapo picha hiyo iliweza kuchukua vichwa vya habari kila mahali.

 

Baada ya hapo watoto hao walichukua nafasi kubwa sana katika mtandao wa Instagram na wakafanikiwa kupata dili ya kusainiwa na kampuni moja ya mamodo.

 

Mapacha hao Leah Rose na Ava Marie ni mastaa wa mtandao wa Instagram kwani wana wafuasi zaidi ya 800,000 na akaunti yao inatambulika.

Mama yao, Jaqi,  anasema amekuwa akipata simu na meseji za watu wanaohitaji kukutana na watoto hao mapacha.

Mapacha hao wenye umri wa miaka nane wamefanikiwa kusajiliwa katika kampuni kubwa mbili ambapo moja ni kampuni ya mavazi ya watoto na nyingine ni jarida.

Dili wanazozipata mapacha hao zimesemekana kuwa ni sita kwa wiki moja.

 

Mama yao anasema wakati mwingine hawaachi watoto wake wafanye kazi wenyewe kwenye kupiga picha zao za mavazi ila huwasaidia kushirikiana kwenye picha hizo kwa pamoja.

 

Wanapenda sana kujaribu kila nguo, wakati mwingine wanatengeneza nywele zao na hata make-up wanapata,” alisema mama wa mapacha hao.

 

Mama huyo pia amesema nje ya dili za kibiashara huwa anachukua muda wa saa tano pia kuwazungusha wanaye jijini Los Angeles.

 

 

Mapacha  bado wanaendelea kuchukua matangazo kwa yeyote kwa sababu wanataka waendelee kukua na nyota hiyo ambayo mama yao alipenda iwatembelee toka mwanzo.

 

Comments are closed.