The House of Favourite Newspapers

CHADEMA Haijaridhika na Maamuzi ya Mahakama

0

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo, kimesema hakijaridhika na uamuzi uliotolewa na Jaji Kiongozi Mustapha Siyani katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wao Freeman Mbowe pamoja na wenzake watatu.

 

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika, ambapo ameeleza kwamba kama Chama wanatafakari hatua za kuchukua ili haki itendeke dhidi ya Kiongozi wao.

 

Mnyika ameeleza hayo mudfupi baada ya uamuzi wa mapingamizi mawili yaliyotolewa na Jaji Siyani kwa kueleza kwamba mapingamizi ya maelezo kuchukuliwa baada ya masaa manne kupita na pasipo hiyari ya mshtakiwa.

 

Katika maamuzi yake amesema kwamba mapingamizi hayo yamekosa mashiko, na kwamba maelezo yalichukuliwa ndani ya masaa manne, na pia maelezo yalitolewa na mshtakiwa wa pili kwa ridhaa yake.

 

“Uamuzi mdogo uliotolewa na Jaji leo hatujaridhika nao, uamuzi katika mapingamizi yote mawili. Jaji ambaye kwa sasa ni Jaji Kiongozi hajaonyesha uongozi wa kutenda haki. Tutakwenda kukutana kama chama kutafakari kwa kina wakati Mawakili wakishauriana na Watuhumiwa,” John Mnyika, Katibu Mkuu CHADEMA.

Leave A Reply