The House of Favourite Newspapers

Lindi: Dereva wa Lori Afariki Mikononi mwa Polisi

0

Jeshi la Polisi mkoani Lindi, wametolea ufafanuzi wa tukio la dereva wa lori aliyefariki mikononi mwa polisi mnamo Oktoba 17, 2021.

 

Taarifa ya Polisi inaeleza kuwa, katika eneo la Jamhuri manispaa ya Lindi majira ya saa 23:30 usiku, polisi walisimamisha lori lenye namba T992 DJZ na tela namba T693 DKA lakini dereva Ibrahim Said anayesadikiwa kuwa na umri kati ya (30-35) akiwa na mwenzie alikaidi amri hiyo na kumgonga polisi katika kizuizi cha Polisi SIDO.

 

Said alimgonga askari polisi aliyekuwa akisimamisha gari hilo na kisha kwenda kuvamia mti, kisha kushuka na kumfuata askari mwingine ambaye alikuwa na silaha na kisha kumchoma visu sehemu mbalimbali za mwili kwa lengo la kupora silaha lakini askari walifanikiwa kumthibiti baada ya kumjeruhi kwa risasi iliyopelekea kifo chake.

 

Majeruhi wawili akiwemo afisa mmoja na askari wawili wanaendelea vizuri baada ya kufikishwa hospitali ya Sokoine kwa matibabu. Jeshi la polisi mkoani Lindi limetoa wito kwa wananchi kutii sheria bila shuruti.

Leave A Reply