The House of Favourite Newspapers

CHADEMA: Katiba Mpya Haina Lengo la Kuwatoa CCM Madarakani, Waache Kuogopa -Video

0

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema uamuzi wa kudai katiba mpya, siyo kwa lengo la kuing’oa CCM kutoka madarakani, bali lengo ni kuhakikisha Watanzania wanakuwa na maisha bora.

Hayo yamesema na Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chadema katika mahojiano na Kipindi cha Front Page kinachorushwa na Kituo cha Redio cha +255 Global Radio na Global TV ambapo amesema mahali pa kuanzia kwenye kupata katiba mpya, ni kwenye Rasimu ya Jaji Warioba.

 

Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chadema

Kigaila amesema hiyo ni kwa sababu rasimu hiyo ndiyo yenye maoni ya Watanzania nchi nzima, na kwamba mahali walipofarakana na CCM ni baada ya kuona maoni ya wananchi yanapinduliwa kwenye bunge la katiba na badala yake yanawekwa maoni ya CCM na ndipo vyama vya upinzani vilipoamua kuugomea mchakato huo.

Kigaila akiwa kwenye picha ya pamoja na watangazaji wa Front Page, (kutoka kushoto) Richard Manyota, Mansoor Malick na Richard Ngaila

Ameongeza kwamba Chadema imeshawasilisha serikalini njia sahihi zitakazowezesha kupatikana kwa katiba mpya na kuongeza kuwa lengo la katiba mpya, siyo kuitoa CCM madarakani bali kuboresha taasisi ya urais na mifumo ya uongozi wa nchi na kwamba kama lengo lingekuwa ni kuiondoa CCM madarakani, basi wangejikita kwenye tume huru ya uchaguzi pekee.

 

Amekitaka chama tawala cha CCM kutoogopa mchakato huo kwani lengo ni kurudisha mamlaka kwa wananchi na kuboresha maisha ya Watanzania wote bila kujali itikadi zao za vyama.

Leave A Reply