The House of Favourite Newspapers

Kinata MC: Mimi Ndiyo wa Kwanza Kuimba Singeli kwa Kiingereza Bongo

0
Kinata MC, msanii wa muziki wa singeli

Msanii wa singeli, Suleiman Kasembe almaarufu Kinata MC, amesema yeye ndiyo msanii wa kwanza wa muziki wa singeli nchini kuja na ubunifu wa kuimba kwa kuchanganya na Kiingereza kwenye nyimbo zake za singeli.

MC Kinata amesema ubunifu huo aliokuja nao, umekuja kuubadili muziki wa singeli na kuupa ladha ya tofauti inayoonesha kupendwa na watu wengi zaidi.

 

Pia amezungumzia mambo mengine mengi kuhusu maisha yake, likiwemo suala la kutomjua baba yake tangu amezaliwa na jinsi alivyoweza kulihimili mpaka sasa amekuwa mkubwa na kueleza kwamba awali suala hilo lilimsumbua sana lakini kwa sasa ameshazoea.

Mahojiano kamili yapo Global TV.

 

 

 

Leave A Reply