The House of Favourite Newspapers

Chadema Wampigania Lema, Wataka Apelekwe Mahakamani Haraka

Godbless-Lema-ArushaARUSHA: Chadema imetua Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kufungua kesi dhidi ya Mwanasheria Mkuu na Jeshi la Polisi ikitaka mbunge wa jimbo hilo, Godbless Lema apelekwe kortini.

Chama hicho kinaiomba Mahakama hiyo kuwaamuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali na maofisa wanne wa Jeshi la Polisi akiwamo IGP, kumpeleka mahakamani mbunge huyo kwa madai amepitiliza muda wa kisheria wa kushikiliwa mahabusu na jeshi hilo.

Mbunge huyo machachari wa Chadema amekuwa rumande tangu Jumatano alipokamatwa mjini Dodoma alikokuwa akihudhuria vikao vya Bunge na kuwa kitendo cha polisi kumshikilia zaidi ya saa 24 ni kinyume cha sheria kwani amekuwa ndani zaidi ya saa 175, hivyo kinamnyima mtuhumiwa haki za kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua kesi hiyo, Wakili wa Chadema, John Mallya amesema leo itapangiwa jaji wa kuisikiliza na siku ya kuanza.

Comments are closed.