The House of Favourite Newspapers

CHADEMA Kuwapa Mazingira Bora Wafanyabiashara

0

MGOMBEA mwenza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Salum Mwalimu, ameahidi kuwawekea mazingira mazuri wafanyabiashara wote.

 

Alitoa ahadi hiyo jana mjini Babati Mkoa wa Manyara wakati akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Motel Papaa katika kampeni zinazoendelea kwa ajili ya uchaguzi mkuu.

 

“Suala la kukadiriwa kodi kwa macho ni marufuku na maofisa wa TRA (Mamlaka ya Mapato nchini) wengine hawajawahi kumiliki hata kibanda cha nyanya,” alisema Mwalimu.

 

Aliongeza kwamba mfanyabiashara hawezi kulinda biashara kwa kupigwa nyundo kichwani na maofisa wa bodi wasiokuwa waaminifu akisisitiza kwamba haki za wafanyabiashara zinatakiwa kulindwa kwa kuwa wanatunza kumbukumbu za biashara zao.

 

Akitoa ahadi hiyo alisema wengi wa wafanyabiashara hao wanafungua maduka yao kwa mazoea huku akiwahakikishia kufurahia kipindi cha uongozi wa (mgombea urais wa chama hicho), Tundu Lissu,iwapo watampigia kumwezesha kushika nafasi ya urais.

 

Mwalimu alitumia fursa hiyo kumuombea kura Lissu, wabunge na madiwani wa upinzani hasa wa Chadema.

Na John Walter- BABATI

Leave A Reply