The House of Favourite Newspapers

Chadema Yalia na Serikali Kuhusu Mfumuko wa Bei Nchini

0
Freeman Mbowe akizungumza na wanahabari leo.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema Serikali imeshindwa kusimamia mfumuko wa bei ya chakula nchini kwa sababu haitambui umuhimu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).

Mbowe amesema mwakà 2015, NFRA ilihifadhi tani 446,000 za chakula lakini kufikia mwaka huu wakala huyo amehifadhi tani 74,826 za chakula.

 

Mbowe amesema chakula kinapanda bei kwa sababu hakuna mkakati wowote wa Serikali kuwainua wakulima kwa kuwapatia pembejeo za kilimo.

“Bei ya mahindi kwa mwakà 2015 ilikuwa 2015 lakini mwaka huu imefika zaidi ya 90,000. Wananchi wanapata shida kwa sababu Serikali yao imewatupa wakulima.”

 

Chadema Waicharukia Serikali Ugumu wa Maisha, Sikiliza Povu la Mbowe

Leave A Reply