The House of Favourite Newspapers

Majaliwa Aagiza TAKUKURU Kukamatwa Viongozi Jiji la Mbeya kwa Ubadhirifu

0
Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa.

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mbeya kuwakamata, kuwahoji na kisha kuwafikisha mahakamani mara moja viongozi wa wa jiji hilo kwa ubadhirifu na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Tsh bilioni 63.

 

Majaliwa ameagiza kukamatwa kwa waliowahi kuwa wakurugenzi watatu na Kaimu Mkurugenzi mmoja wa Jiji la Mbeya, Meya Mstaafu wa jiji hilo, wahasibu wawili na wajumbe wote wa bodi walioshiriki kuidhinisha fedha za Mradi wa Soko la Mwanjelwa kwa kuisababishia hasara kubwa halmashauri ya jiji hilo.

 

Agizo hilo linafuatia watajwa kuongeza gharama za ujenzi wa soko hilo kutoka shilingi bilioni 13 hadi kufikia zaidi ya shilingi bilioni 19 na hivyo halmashauri kutakiwa kulipa deni hilo na riba inayofikia zaidi ya shilingi bilioni 63.

ILIKUPITA HII? Majaliwa Atoa Siku 2 Madiwani Wamalize Tofauti Zao Mbeya 

Leave A Reply