Chama Agawa Tuzo Kwa Mastaa Simba Ligi Kuu Bara
CLATOUS Chama, kiungo mshambuliaji ndani ya kikosi cha Simba ameweka wazi kuwa ikiwa atakosa tuzo ya kiungo bora ndani ya Ligi Kuu Bara kisha wakachukua nyota wengine anaocheza nao ndani ya Simba, kwake itakuwa furaha.
Jina la Chama ni miongoni mwa mastaa wanaowania tuzo ya kiungo bora ndani ya ligi msimu wa 2022/23 akiwa pamoja na Mzamiru Yassin na Saidi Ntibanzokiza wote wanakipiga ndani ya Simba.
Kiungo huyo ni namba moja kwa nyota wenye pasi nyingi za mabao akiwa nazo 14 kibindoni, ametupia mabao manne. Kahusika katika mabao 18 kati ya mabao 66 yaliyofungwa na Simba iliyo nafasi ya pili na pointi 67.
Nyota huyo amesema: “Kuwa katika orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ni jambo zuri lakini muhimu kuona wachezaji wenzangu hili wanalipokeaje.
“Ukweli ni kwamba hatujawa na msimu mzuri uwanjani kutokana na matokeo ambayo tumeyapata hivyo kwa yalitotokea tunafanyia kazi.
“Nimeona kuna majina matatu kutoka Simba ikiwa ni mimi, Mzamiru Yassin na Saidi Ntibanzokiza. Ninaamini wakichukua itakuwa furaha kubwa pia,” alimaliza Chama.
Stori na Lunyamadzo Mlyuka