The House of Favourite Newspapers

Chama Aipa Presha Yanga Ligi Kuu Bara

0

KIUNGO fundi raia wa Zambia Clatous Chama ametamba kuwa wana malengo makubwa kwenye msimu huu na kubwa ni kuutetea Ubingwa wa Ligi Kuu Bara na kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Kauli hiyo huenda ikawatisha wapinzani wao wakubwa Yanga waliokuwepo kileleni katika msimamo wa ligi wakiwa na pointi 49 wakifuatiwa na Simba wenye 42.

 

Simba jana ilitarajiwa kujitupa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam saa kumi kuvaana dhidi ya Al Ahly ya nchini Misri katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Chama alisema kuwa wanafahamu cha kufanya ili kutimiza malengo yao ya kutetea makombe yao wanayoyashikilia ambayo ni ligi na FA.

Chama alisema kwa upande wao wachezaji watatimiza malengo yao waliyojiwekea katika msimu huu, hivyo kila mmoja atatimiza wajibu wake.

 

“Kama wachezaji tunapambana na kutimiza wajibu wetu uwanjani, hivyo Wanasimba wote ni wakati wao wa kwa sasa kujitokeza uwanjani kwa ajili ya kutusapoti.

 

“Tunafahamu umuhimu mkubwa wa michezo yote ya ligi na michuano ya kimataifa na kikubwa tunatakiwa kufanya vizuri katika kila mashindano yaliyopo mbele yetu.

 

“Tutahakikisha tunapambana kuutetea ubingwa wa ligi na hilo ndiyo moja ya malengo yetu, hakuna kinachoshindikana kwetu katika msimu huu,”alisema Chama.

STORI: WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Leave A Reply