Chama Amaliza Ugonjwa wa Manula Mazoezini

Staa wa Simba, Claytous Chama

KIUNGO staa wa Simba, Claytous Chama jana alitumia muda mwingi mazoezini kudili na tatizo la Aishi Manula kufungwa mabao kwa mashuti ya mbali.

 

Chama alichukua mpira na kukaa nao katikati ya uwanja kumfanyia mazoezi kipa huyo kwa dakika kadhaa na baadaye akamuonyeshea dole akimaanisha kwamba ameanza kuimarika.

 

Manula msimu uliopita ambapo Simba iliruhusu mabao ya kufungwa 15 kati ya hayo Manula aliyofungwa yalikuwa ni yale ya nje ya 18 kama ambavyo alifungwa na mshambuliaji wa Alliance Zabona Khamis kwenye ushindi wa mabao 5-1 pia hata msimu huu mbele ya JKT Tanzania wakati Simba ikishinda mabao 3-1 alitunguliwa bao la mbali.

 

Kwenye mazoezi yaliyofanyika jana viwanja vya Gymkhana baada ya Kocha wa Makipa Mwarami Mohamed kumaliza programu yake alimshtua Chama na kumpa mpira amalize kazi.

 

Chama bila hiyana akiwa katikati ya uwanja alianza kumpigia mashuti makali Manula ambaye alipangua mashuti mawili kati ya manne huku mawili akiyapaisha.

 

Habari kutoka kwenye benchi la ufundi ni kwamba zoezi hilo litakuwa endelevu mpaka Manula atakapoimarika.

STORI NA MUSSA MATEJA NA LUNYAMADZO MLYUKA, Dar

ZESCO UNITED Watua USIKU wa MANANE, KUMENYANA na YANGA SC


Loading...

Toa comment