The House of Favourite Newspapers

Chama Shujaa Simba Afunga Mabao Mawili dhidi ya Power Dynamos

0

KIUNGO mwenye ufundi mwingi mguuni, Clatous Chama, jana aliibuka shujaa ndani ya kikosi cha Simba baada ya kufunga mabao mawili katika sare ya 2-2 dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.

Chama alifunga mabao hayo dakika ya 58 na 90+2, yote yakiwa ni ya kusawazisha baada ya Power Dynamos kutangulia wakati wote.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Levy Mwanawasa, Ndola, Zambia, Simba ilikuwa na wakati mgumu baada ya wenyeji wao kupata bao dakika ya 28 na hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, matokeo yalikuwa Power Dynamos 1-0 Simba.

Kipindi cha pili, Chama akasawazisha dakika ya 58, kabla ya Power Dynamos kuongeza la pili dakika ya 74.

Wakati watu wakidhani mechi imelala kwa Simba kupoteza, lakini haikuwa hivyo kwani Chama tena aliwainua mashabiki vitini katika muda wa nyongeza baada ya tisini kukamilika.

Bao hilo liliibua matumaini ya Simba kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu ambapo malengo yao makubwa ni kucheza nusu fainali ya michuano hiyo ambapo msimu uliopita waliishia robo fainali.

Simba wana wakati wa kujiuliza katika mchezo wa marudiano dhidi ya Power Dynamos utakaochezwa Oktoba Mosi, mwaka huu jijini Dar ambapo wanahitaji ushindi wa aina yoyote, sare ya bao 1-1 au 0-0 ili kutinga hatua ya makundi.

AL MERREIKH VS YANGA (0-2) UCHAMBUZI wa MASHABIKI wa YANGA..

Leave A Reply