The House of Favourite Newspapers

Championi, Sokabet Wapiga Tafu Soka La Ufukweni

0
Timu ya Chuo cha Ardhi dhidi ya Chuo Cha Uandishi wa habari zikitifuana vilivyo katika ufukwe wa Bahari ya Hindi jijini Dar leo.

 

MICHUANO ya Soka la Ufukweni hapa nchini ambayo inadhaminiwa na gazeti namba moja la michezo hapa nchini la Championi pamoja na Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya Sokabet imeanza kutimua vumbi leo Jumamosi.

Mtifuano ukiendelea ufukwe wa Escape One jijini Dar es Salaam

Michuano hiyo ambayo inashirikisha timu 16 inatimu vumbi katika ufukwe wa Escape One jijini Dar es Salaam.

Timu ya Chuo Cha Ardhi wakiwa katika picha ya pamoja.

Hata hivyo, timu za Chuo cha Ardhi na Chuo Cha Sayansi na Teknolojia cha Da es Salaam (DIT)za jijini Dar es Salaam zimefanikiwa kuianza vizuri michuano hiyo ambayo pia inatumika kwa ajili ya kupata wachezaji watakaounda timu ya taifa ya soka la ufukweni.

 

Timu ya Chuo Cha Ardhi imefanikiwa kuifunga timu ya Chuo Cha Uandishi wa Habari cha Dar es Salaam (DSJ) mabao 5-4 huku DIT ikiitandika Lisbon mabao 10-1.

Hata hivyo, Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally ambao ni wachapishaji wa Gazeti la Championi ambalo ni kati ya wadhamini wa michuano  hiyo amesema kuwa lengo kubwa la kudhamini michuano hiyo ni kusaidia mchezo huo wa bichi soka kupiga hatua zaidi.

 

“Tumejitokeza kuonyesha tunaunga mkono michezo na hususan mchezo huu wa soka la ufukweni.

Wahamasishaji wa Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya Sokabet.

“Lakini pia mbali na kusaidia, lengo lingine ni  kuwasisitiza watu kuwa michezo ni muhimu kwa afya pia ni ajira, kwa hiyo wajitokeze kushiriki michezo” alisema Saleh Ally huku pia akiwaomba watu kujitokeza kwa wingi kushuhudia michuano hiyo ambayo itafanyika kwa wiki nne na itakuwa ikitimua vumbi kila siku za Jumamosi na Jumapili.

Timu ya Chuo Cha Uandishi wa habari.

PICHA/HABARI: DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

Leave A Reply