The House of Favourite Newspapers

OFM Yanasa Mijengo ya Mhasibu Takukuru

0
Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Godfrey Lugai anapoishi kwa sasa.

DAR ES SALAAM: Siku mbili baada ya aliyekuwa Mhasibu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Godfrey John Gugai kupandishwa kizimbani kwa makosa kadhaa yakiwemo ya uhujumu uchumi, Kitengo Maalum cha Operasheni Fichua Maovu (OFM) kimezama mtaani na kuibuka na baadhi ya nyumba anazodaiwa kumiliki.

Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Godfrey Lugai.

Katika eneo la Ununio, ambalo kuna mijengo mingi ya bei mbaya na kifahari, OFM iliweza kupata nyumba zaidi ya tano zilizojengwa eneo moja ambazo zote zilidaiwa kumilikiwa na mhasibu huyo ambaye awali aligeuka ‘bingo’ baada ya Takukuru kutangaza zawadi ya shilingi milioni kumi kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwake. Nyumba hizo zilikuwa ni moja ya ghorofa moja na zingine za kawaida, ambazo ukiondoa moja ambayo anadaiwa kuwa ndiyo anayoishi kwa sasa, nyingine zilikuwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake.

“Hapa ndipo anapokaa huyo bwana, ni jirani yetu na ni mtu mzuri tu, hizi nyumba zote ni zake, lakini mwenyewe anakaa ndani ya huu ukuta, kuna bonge la nyumba hapo na bustani ya kufa mtu,” alisema Mwenyekiti wa Mtaa wa Ununio, Moshi Abdallah ambaye alisema Gugai alikuwa pia akishiriki misa katika Jumuiya ya Mtakatifu Hilal.

Mwanzoni mwa wiki hii, Takukuru ilitangaza kumtafuta mhasibu wake huyo, ikidai alikuwa ametoroka nyumbani kwake kufuatia kukosa maelezo ya umiliki wa mali nyingi, zikiwemo nyumba na viwanja katika maeneo mbalimbali nchini.



Lakini siku moja baada ya tangazo hilo, Gugai alijitokeza na kujisalimisha, akikanusha kuondoka nje ya nchi na kusisitiza kuwa yupo tayari kukabiliana na kesi mahakamani. Juzi Alhamisi, mhasibu huyo alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka 43.

Mhasibu Takukuru Akutwa na Mashtaka 44 (Video)

Leave A Reply