The House of Favourite Newspapers

Changanya Liwa, Nyanya na Tango Kuondoa Weusi!

0

Nimekuwa nikipokea malalamiko ya wanawake wengi wanaojipenda wakieleza jinsi wanavyosumbuliwa na tatizo la kuwa na weusi f’lani kwenye magoti na nyuma ya mikono kwenye kiwiko.

Kimsingi zipo njia nyingi za kuondokana na tatizo hilo lakini leo nimeamua kukuletea mchanganyiko wa vitu ambavyo ni rahisi kuvipata nyumbani kama vile juisi ya limao, tango, nyanya na liwa.

 

Jinsi ya kutengeneza

Chukua juisi ya nyanya kijiko kimoja, tango kijiko kimoja, limao kijiko kimoja na unga wa liwa kijiko kimoja.

Ukishapata mchanganyiko huo, paka eneo lililoathirika kisha acha pakauke halafu sugua ule mchanganyiko wako. Baada ya hapo osha kwa maji ya vuguvugu.

Kama huna vifaa hivyo nilivyovitaja hapo juu, chukua mafuta ya mzaituni, maziwa na unga wa dengu, changanya na mchanganyiko huo unaweza pia kukusaidia kuondoa weusi wa sehemu nilizotaja.

Leave A Reply