The House of Favourite Newspapers

Chanzo cha Matatizo ya Uzazi na Mamna ya Kuyakabili -3

MSOMAJI wangu, bado naendelea na mada hii ambapo leo nitageukia kipengele cha maambukizi ya virusi vinavyosababisha matatizo katika uzazi.

Kuna aina nne ya virusi ambao huenezwa kwa njia ya ngono na ni hatari kwa afya ya viungo vya uzazi. Aina hizi ziko kwenye lugha ya kigeni ambazo ni Human Pssapilloma Virus (HPV), Harpes, Hepatitis na HIV.

 

Virusi vya HPV mara nyingi huwa havionyeshi dalili yoyote, huenezwa kwa tendo la kujamiiana kwa kugusana ngozi, kwa njia ya kinywa, ukeni na haja kubwa. Aina hii ya virusi husababisha magonjwa ya vioteo na saratani ya shingo ya kizazi.

Kansa zitokanazo na maambukizi haya ni kansa ya ukeni kwa nje au vulva, kansa ya ukeni kwa ndani na shingo ya kizazi, kansa ya uume na kansa ya njia ya haja kubwa. Pia saratani ya koo, baadhi zinasababishwa na HPV kutokana na mapenzi kwa njia ya mdomo ‘oral sex’. Uchunguzi na tiba hufanyika katika hospitali za mikoa.

 

Genital herpes ni ugonjwa uitwao malengelenge na husambaa kwa njia ya kugusana miili, kinywa, ukeni na haja kubwa.

Dalili zake ni kutokwa na malengelenge kama umeungua au wengine huita vidonda vya homa. Hutokea na kupotea vyenyewe, wakati mwingine hupasuka na kuacha vidonda vyekundu.

Uchunguzi wake hufanyika hospitali. Tiba huchukua muda mrefu kwani mara nyingi huwa ngumu kutibika. Athari kubwa ni kumwathiri mtoto anapozaliwa hivyo mama hushauriwa ajifungue kwa upasuaji.

 

Homa ya ini au hepatitis ni mojawapo ya tatizo kubwa ambalo mtu hawezi kujifahamu. Homa hii ya ini imegawanyika katika sehemu kuu tatu, kuna hepatitis A,B n C.

Virusi vya hepatitis hushambulia ini na kusababisha ugonjwa wa ini wa kudumu mwishoni au hufanya mgonjwa apate kansa ya ini. Ugonjwa wa hepatitis A na B huzuilika kwa chanjo maarufu kama chanjo ya manjano.

 

Hepatitis C huwa haina chanjo. Homa ya ini huwa haina tiba. Hepatitis A husambaa kwa njia ya kinyesi kwa hiyo usafi wa mazingira ni muhimu.

Hepatitis B huenezwa kwa njia ya damu au majimaji ya mwilini .

Hepatitis C nayo husambazwa kwa njia ya damu na majimaji mwilini.

 

Jinsi ya kujikinga na maambukizi ya homa ya ini kwanza ni kupata chanjo dhidi ya hepatitis B.

Epuka ngono zembe, epuka kushirikiana sindano, usishirikiane na mtu vifaa vya kutogea masikio au vifaa vya tatuu na hata vifaa vya kunyolea. Usishirikiane miswaki na nyembe.

Maambukizi ya Ukimwi au HIV husababisha ugonjwa uitwao AIDS ambao kwa kirefu ni Aquared Immune deficiency Syndrome.

 

AIDS ni upungufu wa kinga mwilini ambao kiswahili tunauita Ukimwi. Kupata maambukizi ya HIV ni hatua ya awali ya tatizo ila kupata Ukimwi ni hatua ya juu sana.

Watu wengi wanaweza kupata maambukzi ya virusi lakini wachache wanaweza kupata Ukimwi. Ili kuepuka HIV ni kujisalimisha toka katika vyanzo vya maambukizi mfano ngono au zinaa na kuzingatia kanuni za kuepuka magonjwa yote ya zinaa. Mtu hupata magonjwa ya zinaa .

Maambukizi ya virusi vya Ukimwi husambaa kwa njia kuu nne ambazo ni, kwa njia ya majimaji ya mwilini na ngono bila kinga. Hakuna tiba ya Ukimwi na ukiupata utakuwa nao maisha yako yote.

Comments are closed.