The House of Favourite Newspapers

Chanzo Cha Vita Ya Palestina Na Israeli, Vita Ya Kidini Ukristo Na Uislamu?-Video

0

Bila shaka baadhi ya watu hawafahamu kwamba japokuwa taifa la Israel halipo katika bara Ulaya, limekuwa likishiriki katika michezo ya Ulaya kwa zaidi ya miaka 45 sasa. Lakini kumekuwa na wito wa kutohudhuria ghafla hiyo kutoka kwa wakosoaji wa Israel kutokana na sera yake dhidi ya Palestina katika eneo la Gaza na hilo ndilo chanzo ya vita kati ya mataifa hayo na sio dini.

 

Mgogoro kati ya Israel na Palestina umekuwepo kwa miongo kadhaa sasa na swala la umiliki wa ardhi ndio limetajwa kuwa chanzo. Uingereza ilichukua na kudhibiti eneo linalojulikana kama Palestine baada ya mtawala wa eneo hilo la mashariki ya kati mfalme wa Ottoman kushindwa katika vita vya duniani vya kwanza.

 

Ardhi hiyo ilikuwa ikimilikiwa na Wayahudi walio wachache na Waarabu walio wengi. Uhasama baina ya makundi hayo mawili ulianza wakati jamii ya kimataifa ilipoipatia Uingereza jukumu la kuwapatia makaazi Wayahudi katika eneo la Wapalestina.

 

Kwa upande wa Wayahudi eneo hilo lilikuwa la mababu zao, lakini Waarabu Wapalestina pia nao walidai kumiliki ardhi hiyo na hivyobasi wakapinga mpango huo.Kati ya mwaka 1920 na miaka ya 1940, Idadi ya Wayahudi iliowasili katika eneo hilo iliongezeka, huku wengi wakitoroka kuuawa barani Ulaya (Ujerumani) na kutafuta eneo la kuishi baada ya mauaji ya Holocaust ya vita kuu ya dunia.

Leave A Reply