The House of Favourite Newspapers

Mfalme Wa Cocaine Aliyetikisa Dunia-Video

0

Escobar alizaliwa Desemba 1, 1949 katika Mji wa Rionegro nchini Colombia na baadaye, familia yao ilihamia Medellin ambako ndiko alikosomea na kukulia.

 

Baada ya kumaliza masomo yake ya ngazi za chini, alijiunga na Chuo Kikuu cha Universidad Autónoma Latinoamericana kilichopo katika Mji wa Medellín aliokuwa akiishi.

 

Hata hivyo, hakumaliza masomo yake, badala yake akaingia mtaani na hapo ndipo alipoanza kujiingiza kwenye matukio ya kihalifu, ikiwemo kuuza mihadarati, kuuza tiketi feki za michezo ya bahati nasibu pamoja na kujihusisha katika wizi wa magari.

 

Aliendelea kuzama kwenye matukio ya kihalifu ambapo mwanzoni mwa miaka ya 1970, alianza kushirikiana na wafanyabiashara wakubwa wa madawa ya kulevya, ambao walikuwa wakimtumia kusafirisha madawa hayo kwa njia za panya.

 

Hakuishia hapo, akawa pia anajihusisha na matukio ya utekaji nyara, ambapo yeye na wenzake walikuwa wakiwateka watoto wa matajiri na kudai fidia ya mamilioni ya fedha.

Leave A Reply