The House of Favourite Newspapers

Chawote Yaendelea Kumwaga Mkwanja Kwa Wateja wa Tigo

0

Dar es Salaam 14 Julai 2023: Washindi wa zawadi ya shilingi milioni  moja katika Kampeni ya Chawote kutoka mtandao wa Tigo wamesema zawadi walizozipata zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Wakizungumza wakati wa kukabidhiwa zawadi zao leo Julai 14 jijini Dar es Salaam, mshindi Kurwa Abdllah ambaye ni mama lishe kutoka  Kigamboni Dar amesema fedha hizo zitaongeza thamani kwenye biashara yake huku, Retuta Matei anayefanya biashara ya kuuza mkaa Mabibo Dar akisema fedha hizo zimemfikia wakati muafaka.

Kwa upande wao washindi wengine Fatuma Khatibu mkazi wa Buza Dar anayefanya biashara ya saluni amesema fedha hizo zitamsaidia pakubwa kutanua wigo wa biashara yake kauli iliyoungwa mkono na  mshindi mwingine, Peter Okoka Mwasandube kutoka Kurasini Dar.

Kampuni ya Tigo imekuwa ikitoa zawadi mbalimbali kwa watumiaji wa huduma mbalimbali za mtandao huo katika kampeni maalumu ya Chawote inayotarajiwa kudumu kwa siku 90.

Leave A Reply