The House of Favourite Newspapers

Chege, Nature Wafunguka Walivyomaliza Bifu Lao -Video

0

MSANII mkongwe wa Bongo Fleva ambaye bado anafanya vizuri kwenye game ya muziki, Juma Kassim maarufu Juma Nature na Msanii Chege Chigunda leo Mei 26, 2021 wamefika  katika kipindi cha Bongo 255 kinachoruka kupitia Global Radio kufanya mahojiano na wamefunguka jinsi walivyomaliza ugomvi wao waliokuwa nao kupindi cha nyuma.

Kwa upande wake Nature amesema kwa sasa wao ni watu wazima na wajikita zaidi kufanya kazi na mashabiki wakae mkao wa kula”Niliwaza zamani sana kukaa na Chege na kufanya kazi, Sasa tumeshakuwa watu wazima na tunajitambua, tutapiga kazi, mashabiki wajiandae.”

 

Chege amesema ujio wao kwa sasa umeangalia zaidi nini soko linahitaji “Mimi na Chege tumeanza game kitambo watu wanatufahamu, lakini kutengeneza hii ngoma ya pamoja tumeangalia soko linataka nini, watu wametu-miss sana, lazima tufanye kitu wanachokitaka, hatuendi nje tunafanya kitu ambacho jamii wanakihitaji.”

 

“Mimi ndio nilikuwa wa kwanza kumtafuta Nature miaka hiyo, niliona nikifanya kazi na huyu jamaa ipo siku nitakuja kutusua, nikapanga kolabo naye ikaleta ukaribu, Nature naye akaniona akaomba Management yake niende naye kwenye tour Uganda.” 

Kuhusu suala la kufanya ya ngoma na urejeo wa kundi la TMK Family, Chege amesema kwa sasa hawezi kumzungumzia Temba ila wakati sahihi ukifika atalizungumzia”Siwezi kuzungumzia urejeo wa Kundi la TMK bali naweza kuzungumzia combination ya Chege na Nature, sisi tunaamini tumeunganishwa na Mungu, na tukigfanya kazi inakuwa nzuri, chemistry yetu haijawahi kukosewa tangu tumeanza muziki. Ngoma zetu zinakuwa ni za kipekee.”

 

“Tuna mipango mingi ya kuifanya hii project ya Chege na Nature kuwa ya kipekee, hatutaiacha iwe nyepesi nyepesi, combination yetu itaacha alama.”

 

Chege ambaye kwa pamoja na Mhe. Temba waliwahi kuteka nyoyo za mashabiki amesema kwa sasa hawezi kumzungumzia Temba kwani sio wakati wake

“Menejimenti yangu imenizuia kuzungumzia masuala hayo, napaswa kuzungumzia project yangu na Nature, sio vizuri kuanza kuzungumzia watu kwa sasa, wakati wake ukifika tutazungumza.”

 

 

Leave A Reply