The House of Favourite Newspapers

Balaa la Twanga Pepeta Usiku wa Manane

0

 

Kiongozi wa wanenguaji Twanga, Super Nyamwela katikati akionesha makamuzi na wanenguaji Chiku Kasika (kulia) na Maria Soloma.                                                                                                   

BENDI ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ inayotamba na wimbo wake mpya wa Mapenzi Sigala Kali, usiku wa kuamkia jana (Jumamosi) ilipiga bonge la shoo ndani ya kiwanja cha Green Palm kilichopo Kunduchi Jijini Dar.

Mtunzi wa wimbo wa Mapenzi Sigala Kali, Chaz Baba (kushoto) na Mkurugenzi wa bendi hiyo, Luiza Mbutu wakiwajibika jukwaani. Nyuma yao, Shaka Zulu akinogesha mambo kwa gitaa.      

Shoo hiyo ilihudhuriwa na nyomi la mashabiki ambapo wapiga vyombo na wanenguaji walifanya makamuzi si ya kitoto.

Repa wa Twanga, Msafiri Diouf akimchagiza shabiki.                    

Mnenguaji mwenye makeke mengi ambaye ni kiongozi wa wanenguaji wa bendi hiyo, Super Nyamwela na wanenguaji wake nao kama kawaida yao ilikuwa full kudatisha na mastaili yao mapya.

HABARI/PICHA:RICHARD BUKOS /GPL 

Mpiga dram Kirikuu Mashine akifanya yake.                                                                                                       
Mnenguaji Chiku Kasika akiwa amejibinua kimtindo wakati akiwachizisha mashabiki.
Leave A Reply