The House of Favourite Newspapers

Cheki Rose Manfere Alivyotwaa Taji la Miss Tanzania kwa Mbwembwe

0

Mrembo Rose Manfere usiku wa kuamkia leo ametwaa taji la Miss Tanzania kwa mbwembwe na mikogo akiwabwaga wenzake 19 katika shindano lililofanyika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo Posta Jijini Dar.

 

 

Rose alianza kuonesha mikogo yake tangu walipoanza kupita jukwaani na kuonesha vipaji tofauti.

 

 

Katika mpambano huo mgeni rasmi alikuwa Naibu Spika wa Bunge, Akson Tulia ambapo akizungumza mbele ya wageni waalikwa alimuomba muandaaji wa mashindano hayo, Basila Mwanukuzi kuendeleza vipaji vya warembo wengine waliomfuatia Miss Tanzania huyo.

 

Mshindi huyo anayetarajiwa kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya dunia mwakani nchini Brazil, amezawadiwa gari aina ya Subaru.

Angalia picha  

Shoo waliyofungulia.
Naibu Spika Tulia Akson (kulia) akizungumza kwenye shindano hilo kushoto ni muandaaji wa shindano hilo, Basila Mwanukuzi.
Rose akipita jukwaani kwa madaha wakati akiwania taji hilo.
Magreth Mwambi hivi ndivyo alivyopita na vazi la ubunifu.
Msomi wa Shahada ya Udaktari katika Chuo cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki kilichopo Mikocheni Dar, Grace Machibula, akitamba jukwaani.

 

Ruth Benitho akipita kwa madaha.

 

Tamia haka akivinjali jukwaani.
Msomi wa Shahada ya Udaktari kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, Grace Machibula katika vazi jingine.
Tambo za jukwaani hazikuwa za kitoto.
Hawa ndiyo waliofanikiwa kuingia tano bora na anayejibu maswali ndiye Rose Manfere aliyetwaa taji la Miss Tanzania.
Miss Tanzania aliyemaliza muda wake, Silvia Sebastian akimvisha taji hilo Miss Tanzania mpya, Rose Manfere.

 

Rose akipunga mkono kwa furaha baada ya kuvishwa taji.
Akiwa ndani ya gari lake baada ya kukabidhiwa.
Muonekano wa gari alilokabidhiwa.           HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL
Leave A Reply