The House of Favourite Newspapers

Chelsea Kumbakiza Lukaku Mazima Inter Milan, Waongeza Mkataba wa Mkopo Wake

0
Romelu Lukaku mshambuliaji wa Chelsea aliyepelekwa kwa mkopo Inter Milan ya Italia

KLABU ya Chelsea imeripotiwa kufikiria uwezekano wa kumbakiza kwa mkopo wa mwaka mwingine zaidi mchezaji wake Romelu Lukaku hadi mwisho wa msimu wa 2023/2024.

 

Taarifa hizo zimeibuka ikiwa ni mipango ya klabu hiyo kutaka kuachana na mshambuliaji huyo raia wa Ubelgiji lakini pia ikiwa ni njia ya kutengeneza mazingira rahisi kwa klabu ya Inter Milan kuweza kumudu ada ya usajili ya mchezaji huyo.

Lukaku amerudi Inter Milan kwa mkopo hadi 2023 hukukukiwa na uwezekano wa kuongeza muda wa mkopo hadi 2024

Lukaku alijiunga na Chelsea akitokea katika klabu ya Inter Milan kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 97 kabla ya kushindwa kufanya vizuri na kurudishwa kwa mkopo katika klabu yake ya zamani ya Inter Milan.

 

Tayari Lukaku amekiri kwa mashabiki wa Inter Milan kuwa kitendo cha kuihama klabu hiyo na kujiunga na Chelsea katika majira ya joto ya msimu wa 2021/2022 ilikuwa ni kitendo cha makosa na anakijutia kwani hakutakiwa kufanya hivyo.

Leave A Reply