The House of Favourite Newspapers

Mike Tyson Asema Siku Yake ya Kufa Imekaribia, Atoa Ushuhuda kwa Daktari Wake

0
Mike Tyson Bondia mkongwe raia wa Marekani

MWANAMASUMBWI mkongwe kutoka Marekani, Mike Tyson ameushangaza ulimwengu baada ya kudai kwamba kila mara anapotafakari kuhusu maisha yake siku hizi, anaona ni kama mwisho wake kuwa duniani unakaribia na unakuja kwa kasi mno.

 

Katika moja ya podcast zake za ‘Hotboxin’ With Mike Tyson’ aliyoipakia kwenye ukurasa wake wa YouTube wiki moja iliyopita, Tyson akizungumza na daktari wake mtaalamu wa afya, alisema kwamba huwa anajiangalia kwenye kioo na kuona makunyanzi, mapeto na madoadoa ya majeraha usoni mwake na kujisemea kimoyomoyo kwamba siku zake duniani zinakaribia kikomo.

Tyson aliwahi kuwa moja ya mabondia bora Duniani

Tyson mwenye umri wa miaka 56 anasema kwamba pindi anapojitazama kweney kioo anaona kwamba baadhi ya viungo vyake vya mwili na haswa usoni vinazidi kudorora, jambo lilaloashiria kwamab huenda akaondoka kwenye uso wa dunia hivi karibuni zaidi.

 

“Sisi sote tutakufa siku moja bila shaka. Ninapojitazama kwenye kioo, naona madoa hayo madogo usoni mwangu, nasema, wow! Hiyo inamaanisha kuwa siku yangu ya kumalizika kwa muda wangu duniani inakaribia, hivi karibuni,” Tyson alisema kwa ujasiri na ukakamavu usoni mwake.

 

Katika maongezi hayo ya kipekee yenye uhuru wa kuzungumza wa aina yake, Tyson pia alizungumzia maisha yake kwa undani na kugusia kiasi jinsi anavyoyaona maisha haswa kuelekea ‘mwisho wake duniani’ ambapo alisema kwamba hata amefikia kiwango ambapo hana haja tena na mali ya duniani kama pesa, majumba makubwa na hata magari.

Tyson amesema anauona mwisho wake wa kuishi Duniani umekaribia

“Pesa haimaanishi kitu kwangu. Mimi huwaambia watu kila wakati, wanafikiri pesa itawafurahisha, hawajawahi kuwa na pesa hapo awali – unapokuwa na pesa nyingi, huwezi kutarajia mtu yeyote kukupenda.

 

“Nitakirije mapenzi yangu kwako wakati una $500 bilioni? Unaamini hakuna kinachoweza kutokea. Huamini kwamba benki zinaweza kuanguka. Unaamini kwamba huwezi kushindwa wakati una pesa nyingi, ambayo si kweli. Ndio maana huwa nasema pesa ni hisia potofu za usalama,” amesema Tyson.

 

Mike Tyson alikwa bondia miaka ya tisini na kuelekea miaka ya awali ya 2000 ambapo mapambano yake mengi aliyashinda kwa mkumbo wa kwanza na hivyo kujijengea heshima ya kudumu haswa kutoka kwa Wamarekani.

Leave A Reply