The House of Favourite Newspapers

Chelsea Yatenga Dau Kuzinasa Saini za De Jong na Aubameyang Kutoka Barcelona

0
Frenkie De Jong na Pierre Aubameyang wote kwa pamoja wanatakiwa na Chelsea

CHELSEA wapo tayari kufikia ofa ya United ya Paundi milionmi 72 ambayo waalimpa kiungo wa Barcelona na timu ya taifa ya Uholanzi, Chelsea ambayo inashiriki michuano ya Klabu Bingwa Ulaya, ina nafasi kubwa ya kumpata mchezaji huyo tofauti na Manchester united ambayo inashiriki Europa league.

Thomas Tuchel, Kocha wa Chelsea amefanya kazi na Aubameyang wakiwa pamoja katika klabu ya Borussia Dortmund ya nchini Ujerumani

Aidha mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon Pierre Aubameyang alihamia Barcelona kwa uhamisho huru kutoka klabu ya Arsenal mwezi januari na tayari anahusishwa na kurejea nchini Uingereza mara hii anatarajiwa kuungana na Kocha wake wa zamani Thomas Tuchel katika klabu ya Chelsea hiyo ni baada ya kutua kwa Robert Lewandowski aliyetokea klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani.

 

Ingawa kocha wa Chelsea Thomas Tuchel amekuwa akisita kumzungumzia Aubameyang hadharani kwamba anatamani kufanya kazi tena na mchezaji huyo aliyemfungia mabao 79 katika misimu miwili akiwa Borussia Dortmund taarifa zinadai yeye pamoja na mmiliki mpya wa klabu hiyo Todd Boehly wanafanya kila liwezekanalo ili kukamilisha dili la mshambuliaji huyo

Pierre- Emerick Aubameyang na Frenkie De Jong

wiki iliyopita chelsea walimsajili kiungo wa kati carney chukwuemeka mwenye umri wa miaka 18 kutoka aston villa kwa mkataba wa £20m. pia wamemsajili kipa gabriel slonina mwenye umri wa miaka 18 kutoka chicago fire na winga omari hutchinson mwenye umri wa miaka 18 kutoka arsenal.

Imeandikwa: Danstan Mpili kwa msaada wa mitandao

 

Leave A Reply