The House of Favourite Newspapers

Chelsea Yaiduwaza Man City Yatwaa Uefa

0

MATAJIRI wa jiji la London Chelsea ya Uingereza imeshinda ubingwa wa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya Uefa, baada ya kuifunga Manchester City 1-0 usiku wa kuamkia Mei 30, 2021, goli pekee la Chelsea lilifungwa na mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani Kai Havertz dakika ya 42.

 

Huu ni ubingwa wao wa pili katika historia ya klabu hiyo ambapo ubingwa wa kwanza walitwaa mwaka 2012 kwa kuwafunga Bayern Munich.

 

Mlinzi wa kati wa Chelsea raia wa Brazil Thiago Silva ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa tano kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa misimu miwili mfululizo akiwa na klabu tofauti wengine Marcel Desailly, Paulo Sousa, Samuel Eto’o na Álvaro Morata.

Pia kocha Pep Guardiola amepoteza fainali mbili za mashindano katika historia yake ya kufundisha soka tangu mwaka 2008. Alipoteza fainali ya Copa del Rey msimu wa 2010-11 akiwa na Barcelona na sasa amepoteza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Chelsea.

 

Thomas Tuchel amekuwa kocha wa pili kumfunga Pep Guardiola katika mechi tatu mfululizo za mashindano yote akitanguliwa na kocha wa Liverpool Jürgen Klopp ambaye alifanya hivyo mwaka 2018.

 

Leave A Reply