The House of Favourite Newspapers

Chidinma ahofiwa kupotea

0

Chidinma Ekile

ZIKIWA zimepita wiki chache tangu staa wa muziki kutoka Naija, Chidinma Ekile atemane na lebo iliyokuwa ikimsimamia kazi zake za muziki ijulikanayo kama Capital Hill Records, inadaiwa kuwa staa huyo ameanza kupotea kimuziki.

Inaelezwa kuwa mara baada ya kutemana na Capital, Chidinma alidai kuwa anaelekea Bara la Ulaya kufanya shoo lakini haikuwa hivyo.

Chidinma EkileKwa sasa Chidinma hajulikani yupo wapi, hatokelezei kwenye mitandao ya kijamii, haonekani akipafomu kwenye tukio lolote na hata kutokelezea kwenye jamii.

Mara ya mwisho kuachia wimbo mpya ilikuwa Machi mwaka huu ambapo aliachia Wimbo wa Mama akishirikiana na Mr. Flavour.

Leave A Reply