The House of Favourite Newspapers

Wafanyabiashara Kariakoo kunufaika na huduma za Vodacom

0

????????????????????????????????????

Kaimu Meneja Mkuu wa shirika la masoko Kariakoo,Mrero Mgheni(katikati)akikata utepe kuzindua duka jipya la Vodacom Tanzania”Service desk” lililopo langoni mwa soko kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.Wengine kushoto Mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja wa kampuni hiyo,Brigita Stephen na Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam,Dominician Mkama.

????????????????????????????????????Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam,Dominician Mkama,akimuonesha Kaimu Meneja Mkuu wa shirika la masoko Kariakoo,Mrero Mgheni moja ya  simu aina ya”smart phone”zinazopatika kwa bei nafuu katika duka jipya la Vodacom Tanzania”Service desk” lililopo langoni mwa soko hilo mara baada ya kulizindua rasmi leo jijini Dar es Salaam.

????????????????????????????????????Mkuu wa kitengo cha wateja rejareja wa Vodacom Tanzania,Brigita Stephen na Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam,Dominician Mkama,wakimshuhudia Kaimu Meneja Mkuu wa shirika la masoko Kariakoo,Mrero Mgheni(kushoto)akikata keki kuashiria uzindua wa duka jipya la Vodacom Tanzania”Service desk” lililopo langoni mwa soko kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.

????????????????????????????????????Kaimu Meneja Mkuu wa shirika la masoko Kariakoo,Mrero Mgheni(kushoto)akimlisha keki Maria Shabani,ambaye ni mteja wa kwanza kufika katika duka jipya la Vodacom Tanzania”Service desk” lililopo langoni mwa soko kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam mara baada ya kulizindua rasmi leo,Wengine katika picha  Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam,Dominician Mkama(wapili kushoto)na Mkuu wa kitengo cha wateja rejareja wa kampuni hiyo,Brigita Stephen.

Wafanyabiashara na wateja wa soko kuu la kariakoo wataanza kunufaika na huduma mbalimbali za mawasiliano na za kifedha kwa urahisi zaidi, Kwani kampuni ya Vodacom Tanzania katika kutekeleza mkakati wake wa kusambaza huduma zake karibu zaidi na wateja wake popote walipo leo imezindua duka jipya la kisasa sokoni hapo.

Duka hili ni mwendelezo wa kusambaza huduma ambapo kwa mwaka huu kampuni itafungua maduka sehemu mbalimbali ikiwemo vituo vidogo vya kutoa huduma vipatavyo 500 nchini kote.

Kufunguliwa kwa duka hili kutawarahisishia wafanyabiashara wa maeneo ya Kariakoo na wananchi wanaofika  eneo hilo kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali za Vodacom kwa urahisi.

Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam,Dominician Mkama amesema  kuwa mkakati huu wa kufungua maduka na vituo vya kutoa huduma mbalimbali za kampuni yao umebuniwa ili kuwapunguzia wateja wao adha ya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kupata huduma.

Kwetu Vodacom wateja wetu ni wafalme na tunasikiliza ushauri wao,pamoja na kuwa na maduka mengine na mawakala eneo hili la Kariakoo sehemu  bado tumeona kuna haja ya kuwasogezea zaidi huduma wateja  wazipate popote pale walipo na kwa wakati wowote”.Alisema.

Aliongeza kuwa  kupitia huduma hii ya maduka na  vituo vya mauzo kampuni itazidi kupanua wigo wa ajira nchini kwa kuwa watanzania zaidi ya 1000 watanufaika na mpango huu na  ni utekelezaji wa  moja ya malengo ya kampuni ambayo ni kufanya uwekezaji wenye mwelekeo wa kuwanufaisha watanzania.

Akizindua duka hilo,Kaimu Meneja Mkuu wa shirika la masoko Kariakoo,Mrero Mgheni ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa duka hilo zaidi ya kuipongeza kampuni hiyo kwa kusambaza huduma zake karibu na wateja,aliwataka wafanyabiashara wa soko la Kariakoo na wananchi kwa ujumla  kutumia huduma za mawasiliano za kampuni hiyo kwa ajili ya kurahisisha maisha yao na kutokupoteza muda mwingi kuhangaika kutafuta sehemu za kupata huduma hizo kwani wameletewa huduma hizo karibu zaidi.

Mmoja wa wafanyabiashara katika soko hilo Abdallah Rajabu akiongea kwa niaba ya wakazi wenzake alisema kuwa kufunguliwa kwa duka hilo kutawapunguzia kero wafanyabiashara na wakazi wa eneo hilo  kutembea na kuzunguka katika maeneo mbalimbali kufuata huduma za Vodacom“Tunaishukuru Vodacom kwa kutukumbuka wafanyabiashara wa sokoni hili la Kariakoo kwa kweli tutanufaika sana na huduma zao kama vile M-pesa na zinginezo nyingi”alisema

Leave A Reply