The House of Favourite Newspapers

China: Tuhuma na Matamshi ya Marekani Yatasababisha Vita Baridi

0


China imesema uhusiano baina yake na Marekani unakaribia kiwango cha enzi mpya ya vita baridi, inayochochewa na mvutano kuhusu janga la virusi vya corona, miongoni mwa mengine.

 

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesema jana kuwa Marekani imepatwa na virusi vya kisiasa vya kufanya mashambulizi mfululizo dhidi ya China, na kusisitiza kuwa licha ya hayo, Beijing itaendelea kuunga mkono juhudi za kimataifa za kulitafutia suluhu janga la corona.

 

Rais wa Marekani Donald Trump anaituhumu China kuficha ukweli juu ya mripuko wa virusi vya corona, na anaeneza nadharia ya kwamba virusi hivyo viliponyoka kutoka maabara ya siri ya nchini China.

 

Waziri Yi amesema wanasiasa wa Marekani wametengeneza uvumi kuhusu chanzo cha virusi vya corona, ambao amesema unashika mateka uhusiano baina ya mataifa hayo mawili na kuyasogeza kwenye ukingo wa vita vipya vya baridi.

Leave A Reply