The House of Favourite Newspapers

China Yaanza Mazoezi ya Kijeshi Yasiyo na Kifani Kuizunguka Taiwan

0
Ndege za kivita za China zikizulu karibu na kisiwa cha Taiwan

CHINA imeanza mazoezi makubwa ya Kijeshi ya Baharini na Angani, kuzunguka Kisiwa kinachojitawala cha Taiwan saa chache baada ya Spika wa Bunge la Marekani kuondoka Taipei.

 

Vyombo vya Habari vimeripoti mazoezi ya moto ya kijeshi, katika maeneo ya karibu na Taiwan yaliyoanza saa sita za mchana kwa saa za huko na yataendelaea hadi tarehe 7 Agosti.

 

China ilianza mazoezi ya kijeshi kuanzia Siku ya Jumanne Usiku kufuatia kuwasili kwa Pelosi Spika wa Bunge la Marekani kitendo kilichoikasirisha Beijing.

China imesema haitaiacha Taiwan kuhadaiwa na Marekani

Shughuli za Kijeshi ziliendelea siku ya Jumatano, huku Taiwan ikisema kuwa mazoezi hayo yamekiuka sheria za Umoja wa Mataifa ikisema kuwa vikosi vya Majeshi ya China vimevamia maeneo yake Baharini na Angani na kuiweka kizuizini.

 

Siku ya Alhamisi, Wizara ya Ulinzi ya Kitaifa ilitaja shughuli za kijeshi la China kuwa “hazina mantiki”na nia yake ni kudhoofisha hali ya amani na Utulivu wa Kisiwa hicho.

 

Beijing inadai kuwa Taiwan ni yake na haijaacha matumizi ya nguvu kuchukua uthibiti wa kisiwa hicho, Marekani nia yake ni kukipa kisiwa njia ya kujilinda.

Leave A Reply