The House of Favourite Newspapers

CHLOE: Binti wa Miaka 7 Aliyewaandikia Google Barua ya Kuomba Kazi

Mkurugenzi wa Google, Sandar Pichai

 

KWA dunia ya sasa, kila mtu anatamani akafanye kazi katika Kampuni ya Google YA Marekani kutokana na mishahara mizuri wanayolipa na hata marupurupu yake ni makubwa.

Nchini Uingereza, mtoto Chloe Bridgewater mwenye miaka saba aliamua kumuandikia bosi wa Google hamu yake ya kutamani kufanya kazi kwenye kampuni hiyo. Kama ilivyo kwa watu wengine ambao huambatisha na CV zao, mtoto huyo, kwenye barua yake aliwaambia ujuzi aliokuwa nao katika kompyuta na jinsi anavyotumia tablet kucheza michezo mbalimbali.

Chloe akiwa na baba yake, Andy

Inawezekana mimi na wewe tusingeweza kujibiwa barua zetu lakini bahati kwa Chloe ni kwamba wakati ameituma barua hiyo, mkurugenzi wa kampuni hiyo, Sundar Pichai aliweza kuipata, akaisoma na kuijibu kwa mkono wake.

Katika barua aliyoiandika Chloe, alimwambia kwamba anapenda sana kutumia kompyuta na kucheza michezo katika tablet ya baba yake, ila pamoja na hayo, anatamani sana atakapokua awe muogeleaji katika mashindano yote ya Olympic yatakayokuwa yakifanyika kipindi hicho.

Google waliipokea barua yake na mkurugenzi huyo akamwambia kwamba kwanza asome, akishamaliza basi wataweza kumpatia kazi kama anavyotaka kitu kilichomfanya mtoto huyo kuanza kusoma kwa bidii kwa kuamini kwamba hao baadaye atakuwa mfanyakazi mpya wa Google.

Barua aliyoandika Chloe

Mzazi wa Chloe, Andy mara baada ya kuona Google wameijibu barua ya mtoto wake, akaichukua na kuiposti katika Mtandao wa LinkedIn na kueleza ni jinsi gani barua ya majibu ya Google ilivyobadili maisha ya mtoto wake.

“Chloe alikata tamaa baada ya kupata ajali ya gari miaka kadhaa iliyopita lakini baada ya kupokea barua kutoka Google tena ikiwa imesainiwa na Sandar Pichai mwenyewe, imemuhamasisha na kumtia nguvu kwa kuona kila kitu kinawezekana.

Barua aliyojibu Sandar Pichai

“Ni mtu anayejali kwa sababu mtu kama yeye ni lazima atakuwa bize sana ofisini kwake ila ameacha yote hayo na kumjibu Chloe, ni kitu kizuri sana,” alisema baba yake Chloe.

Na: Nyemo Chilongani/GPL

 

Comments are closed.